Social Icons

Saturday 7 April 2012

HILI NI PIGO KUBWA KUMPOTEZA STEVEN CHARLES KANUMBA

Kanumba
Steve Kanumba alipata umaarufu mkubwa Afrika

Tasnia ya filamu nchini Tanzania inaomboleza kifo cha msanii maarufu wa filamu nchini  Steven Kanumba ambaye amefariki usiku wa kuamkia Jumamosi nyumbani kwake Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.
Taarifa zilizothibitishwa na mmoja wa ndugu za Marehemu, zinasema kuwa Marehemu Steven Kanumba alifariki majira ya saa nane usiku, muda mfupi baada ya kutokea mzozo kati yake yake na rafiki yake wa kike ambaye ni msanii mwenzake wa filamu.
Taarifa zinasema marehemu alisukumwa na kuanguka na kugonga kichwa chini upande wa Nyuma na kusababisha kifo chake.
Polisi mkoani Dar es Salaam imethibitisha kuwa inamshikilia kwa mahojiano msanii huyo wa kike kutokana na kuhusika na kifo cha Kanumba, ambaye alijizolea umaarufu mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na hadi Afrika Magharibi baada ya kuwashirikisha katika filamu zake baadhi ya wasanii Maarufu wa Kinigeria akiwemo Mercy Johnson na Noah Ramsey.
Marehemu ambaye alizaliwa mwaka 1984, alianza kujipatia umaarufu mwanzoni mwa mwaka 2000 wakati huo akiigiza katika Michezo ya luninga kupitia kundi la maigizo la Kaole Sanaa.
Aliendelea na kuigiza filamu nyingi ambazo zilimpatia umaarufu mkubwa kiasi cha kusafiri mara kadhaa nchi za nje, ambako alitambulika kama mmoja wa wasanii wenye vipaji vikubwa ambaye aliitangaza fani ya filamu nchini Tanzania maarufu kama Bongo Movies.
Tangu kuanza kutangazwa kwa taarifa za kifo chake mapema alfajiri, mamia kwa maelfu ya watu wamekuwa wakimiminika kwa wingi nyumbani kwa marehemu, huku vyombo vingi vya habari vikizipa kipaumbele mara kwa mara taarifa za kifo cha msanii huyo.

 STEVEN CHARLES KANUMBA (1984 - 2012)                                                                                   
Steven Charles Kanumba (8 Januari 1984, Shinyanga - 7 Aprili, 2012) alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchini Tanzania. Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini.

MAISHA
Na ameanza elimu ya msingi katika shule ya Bugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui na baadae kupata uhamisho katika shule moja ya jiji Dar es Salaam iitwayo Dar Christian Seminary. Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Jitegemee

SHUGULI ZA UIGIZAJI
Kanumba ameanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya "90". Ila kufahamika zaidi alianza mwaka 2002 mara tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kama Kaole Sanaa Group.

No comments:

LATEST NEWS

Share

Widgets

 

Total Pageviews