Social Icons

Tuesday 19 June 2012

Msimamo wa Mnyika wa sasa juu ya Kauli yake bungeni!

Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.
Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!

John Mnyika

19 Juni 2012

WEMA SEPETU ANAJIAIBISHA SASA!!

Hivi karibuni baada ya kutokelezea na kipindi cha Take one cha clouds Tv akionesha nyumba yake mpya aliyonunua kwa zaidi ya Tsh. milioni 400 kijitonyama huku akiendelea na kutuonesha baadhi ya magari yake anayomiliki sasa hali imegeuka na kuwa ggumzo hapa Tanzania. Baada ya kuonesha baadhi ya vitu vilivyomo ndani humo na kudai kuwa nyuma hiyo ni yake na ameitengeneza kwa pesa zake, kimeibuka kisanga kingine baada ya kuibuka kwa

wapambe na mmiliki wa nyumba hiyo ambaye ni Mama mtu mzima na kuweka wazi kuwa nyumba hiyo si ya Wema bali amepangishiwa na amelipiwa kiasi cha miezi sita na mtu aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wake na pia bado anadaiwa kiasi kingine cha miezi sita. Na hii kama itakuwa ni kweli basi hawa wanaojiita mastaa wetu wa Bongo hawatakuwa na la maana zaidi ya kujidharirisha,kama kitu si chako kwanini usiweke wazi!!.


Tuesday 12 June 2012

Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Akutana na Ujumbe Wa Wafanyakazi wa TV Oman


Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe.Bihindi Hamad, Mkurugenzi Mipango na Uendeshaji Joseph Kilangi na Mtayarishaji wa Vipindi wa ZBC TV Ahmeid Talibm wakisikiliza Waziri wakati wa mkutano huo. uliofanyika katika Ofisi ya Wizara ya Habari Kikwajuni.

Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mhe Said Ali Mbarouk, akizungumza na ujumbe wa Wafanyakazi wa TV Oman ulipofika ofisini kwake kujitambulisha kwa ujio wao Zanzibar wa kutengeneza Program ya Utalii wa Zanzibar na Majumba ya Mji Mkongwe na sehemu za Historia ya Zanzibar kuitangaza Kitalii Oman, kushoto kwa Waziri Balozi wa Oman Zanzibar Mansoor Al Busaid na Wafanyakazi wa TV Oman.
---

UONGOZI wa Shirika la Utangazaji nchini Oman, umeahidi kulisaidia Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC – TV) katika nyanja mbali mbali, ikiwemo za kiufundi na kitaaluma, ili liweze kuharakisha juhudi zake za kutoka kwenye mfumo wa Teknolojia ya habari wa Analogy na kuelekea ule wa Digital.

Ahadi hiyo imetolewa jana na Uongozi wa Shirika hilo, wakati ulipokutana na kubadilishana mawazo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar, Said Ali Mbarouk, ofisini kwake Mnazi Mmoja.

Ujumbe huo wenye timu ya waandaji wa filamu, upo nchini kwa ajili ya kutayarisha filamu katika maeneo ya kihistoria, hususan Mji Mkongwe, ambapo pamoja mambo na mengine filamu hiyo itaisaidia kuitangaza Zanzibar kiutalii.

Ujumbe huo ambao uliambatana na Balozi mdogo wa Oman nchini, Mansoor Al Busaid, umeahidi kukutana na Menejment ya ZBC, ili kubadilishana uzoefu pamoja na kuangalia maeneo yepi ambapo Shirika hilo linaweza kusaidia kiufundi na kitaaluma.

Mmoja wa viongozi wa Shirika hilo, Ebrahim Al Yahmad alisema ZBC inaweza kunufaika sana kuwepo mashirikiano na Shirika hilo na kuharakisha safari yake ya kuelekea Digital,kwa kuzingatia kuwa tayari Oman inaondoka katika mfumo huo (Digital ) na kuelekea mfumo wa DH.

Alisema Shirika la Utangazaji la Oman, (ambalo lina Waziri wake) limepiga hatua kubwa sana katika nyanja ya mawasiliano ya habari, hivi sasa likiwa tayari limejenga Studio kubwa ya kisasa, huku likiendelea na maandalizi ya program za mafunzo kwa mfumo wa DH.

Alisema katika dhana ya kuendeleza mashirikiano kati ya mashirika hayo mawili, vijana wa Zanzibar wataweza kupata fursa ya kubadilishana uzoefu na wenzao wa Oman na kuona vipi wanafanya kazi.

Katika hatua nyingine, kiongozi huyo alisema hatua ya kuja kwao nchini na kuandaa filamu katika maeneo ya kihistora kutaisaidia sana kuutangaza Utalii wa Zanzibar, kwa kujua kuwa Zanzibar ni eneo bora kwa biashara ya Utalii.

Aidha alimwomba Waziri Mbarouk kusaidia upatikanaji wa nakala za magazeti ya zamani ambayo yaliwahi kuchapishwa hapa nchini, au kumpata mtu ambae anaweza kueleza kwa ufasaha juu ya uwepo wa magazeti hayo.

Mapema Waziri Mbarouk alisema Serrikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu na ndugu zao wa Oman.

Alisema hatua ya Oman TV kuja nchini kwa ajili ya kuandaa filamu maalum katika maeneo ya kihistoria, ni hatua muafaka inayounga mkono juhudi za Serikali katika kuutangaza utalii wa Zanzibar hadi nje ya mipaka na kufanikisha ‘dhana ya utalii kwa wote’.

Alisema mbali na ujumbe huo kuangalia eneo la Mji Mkongwe, pia wapaswa kuangalia maeneo zaidi ya kihistoria, ikiwemo msitu wa Jozani, magofu ya Mtoni, fukwe zenye kupendeza pamoja na magofu ya Mazrui yalioko Chwaka kijiji cha Tumbe, kisiwani Pemba.

Alisema Zanzibar imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya Utalii, na kutoa mfano wa Hifadhi yam situ wa Jozani, wenye kupatikana Kima Punju, wanyama ambao hawezi kupatikana mahala popote pale Duniani, isipokuwa Zanzibar.

Aidha aliyasifia magofu yalioko Chwaka Tumbe, kwa kusema kuwa ni eneo kubwa, linalovutia na lenye historia inayosisimua, likielezwa kuwa ni mji uliopata kuishi watu kutoka Oman kabla ya kuja kwa Wareno.

Akizungumzia kuwepo kwa magazeti ya zamani, Mbarouk alisema kuna idadi kubwa ya magazeti yaliokuwa yakichapishwa hapa Zanzibar miaka mingi iliopita, na kuuahidi ujumbe huo kupata baadhi ya nakala zake pamoja na watu wanaoelewa historia ya kuwepo kwa magazeti hayo.

Na
Abdi Shamnah -
Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar

MAMA WEMA SEPETU AMPA MAKAVU JACKLINE WOLPER!!























Kama mfuatiliaji mzuri wa myenendo ya mastaa wa Bongo utaikumbuka ile kauli ya Ambarozi wa Bongo hapa namzungumzia Wolper ambaye siku kadhaa zilizopita alisikika akitoa kauli ya kwamba "Atamnunulia Wema Sepetu kitanda", Kauli ambayo leo hii tumeona kwenye kipindi cha Take One cha Zamaradi pale Clouds Tv mama huyo akiongea kwa jazba juu ya kauli ya Wolper huku akitoa maneno makali na kuonesha chumba alichomlelea mwanae toka akiwa mdogo hadi alipohamia kwenye nyumba mwenyewe anazoziita za vichochoroni na kusema Kuwa Wolper asijaribu kujifananisha na mwanae.

FAHAMU KILICHOWAKIMBIZA AY NA MWANA FA KUTOKA B_HITS!

Wakali wawili ambao walikuwa napoteza sana kwa ngoma zao kutoka studio za B Hits chini ya Hermy B ambao kwa kipindi cha takribani miezi sita hivi hawako tena kwenye lebo hiyo wameweza kuweka wazi mapema wiki hii kwanini hawafanyi tena kazi na studio hizo. Wakiongea na Amplifaya wakali hao walithibitisha kutokufanya kazi tena na studio hizo huku wakiweka wazi kuwa kupanda kwa gharama za kurekodi ndani ya studio hizo ndio kikubwa kilichowafanya wakimbie ndani ya
studio hizo na wala hawana tofauti na mmiliki wa studio hiyo.

LATEST NEWS

Share

Widgets

 

Total Pageviews