Social Icons

Monday 24 September 2012

SIMULIZI YA MWEZI HUU- THE COMPANY MAN_MTU KAMPUNI

CHARACTERS:

Jovitha (Main)

john

Ali

Mama Jovitha

Mzee Joachim

Boazi

Pentlez

Jessi

Guest characters

Ande

Nkena

Atupilike

STORY STRUCTURE

Snake ( Middle, mouth to Tail)


LOCATION

Rwanda& Tanzania

(Sehemu zingine si sahihi bali ni za kufikirika

Kwa mf kolbert, K hospital n.k)


MAUDHUI

Mauaji

Rushwa

Tamaa

Ukiukaji wa sheria na haki za binadamu
UTANGULIZI
Jovitha ni Binti wa Kinyarwanda tena mzuri kupita kiasi kikubwa, kutokana na uzuri aliokuwa nao anawavutia wanaume wengi.Anaweza kujiunga na chuo kikuu cha Mzumbe akiwa anasomea sheria, anakuwa na uwezo mkubwa Darasani pamoja na kusumbuliwa na wanaume wengi kutokana na urembo wake tena wa kupitiliza ambao ulimvutia kila anayeitwa mwanaume.

Kutokana na uwezo wake mkubwa darasani anaweza kuwa na marafiki wengi. Pamoja na kuwa na Marafiki wengi pia kulikuwa na marafiki ambao ndani yake walikuwepo wanafiki, wanaomba urafiki ili watimilishe lengo lao na mwisho anafanyiwa unyama kwa kubakwa na wanaume zaidi ya 4 kwa lengo la kumkomoa hiyo yote ni kutokana na msimamo wake dhidi ya wanaume wengi walikuwa na tamaa naye.

Anahapiza kufanya kisasi, na anaanza kufanya mauaji ya kinyama….

Mwisho ambao ni mwanzo wa simulizi hii…Jovitha anaoneka uwanja wa ndege akiwa anaelekea UK kwa masomo zaidi kusomea digrii yake ya pili………ambapo ananguka kwa kuinusa sumu aliyowekewa na ALI. Anakimbizwa hospitalini ambako anaaga Dunia. Lakini jukumu anaachiwa kakae JOHN ili ahakikishe na kuuawa kwa ALI maana alihofia kuuangamizwa kwa familia yake.






SEHEMU YA KWANZA

Hali ya hewa ya Jiji kuu la nchi ya Rwanda Kigali ilikuwa shwali na likiwa na mwanga hafifu wa jua hali ambayo ilisabishwa kuwepo kwa wingu jeupe angani. Hali hiyo ilipendezesha jiji ilo ambalo likuwa linapendeza mno kwa hali ya ukijani wa mti inayoipamba Kigali. Lakini ndani yake alionekana Mrembo Jovitha. J akiwa anaelekea uwanja wa ndege Kolbert akiwa na Safari ya kuelekea masomoni UK –STANFORD UNIVERSITY, pamoja nakuwa na safari hiyo lakini kwake alikuwa hana raha kabisa mawazo yake yalikuwa juu ya Ali maana hakujua kama kweli kama amemmaliza kwani alihitaji kujua kama kweli amemaliza kazi yake juu ya kile alichoapa kuwamaliza waliombaka miaka miwili iliyopita.

Majira ya saa 2:00 asubuhi Jovitha tayari alikuwa uwanjani huku akisindikizwa na familia yake ambayo ilikuwa inaongozwa na kaka yake John kama kichwa cha familia baada yam zee Joachim kufa kwenye ajali mbaya ya moto akiwa kwenye gari yake. Wakati wote huo mama yake Jovitha alikuwa kimya kwani alionekana mwenye mawazo mengi, Jovitha alipoona ali hiyo kwa mama yake alimua kumsihi mama.

Mama punguza mawazo sawa, nakuomba sana” Jovitha alimwambia mama ake huku akimsogelea na kumukumbatia.

Sawa mwanangu nitafuata ushauri wako, Lakini mwanangu nitakuwa mpweke sana kwa kipindi chote cha masomo yako. Nakuomba uwe unanikumbuka pindi utakapokuwa masomoni” Mama Jovitha alimtazama motto wake kwa muda huku machozi yakimdondoka, kwa sasa alionekana wazi ya kwamba haitaji kutengana na Jovitha.

Hey Jovitha shughulika” punguza maongezi kwani hamchokani tu hata kumbikumbi uchokana pale mmoja atakapo toka mbawa” John alimuomba Jovitha huku akichomekea utani wake kama kawaida yake.

“Acha utani wako kaka, huyu ni mama siwezi kumchoka hata kidogo”Jovitha alijibu nakuongeza “Una maana gani unaposema hata kumbikumbi uchokana pale mmoaja atakapotoka mbawa”

“Aaaaah aah nina maana ya kwamba wewe bado una mbawa inakupasa uondoke na kutuachia mama yetu . maana mbawa zake zimetoka hivyo basi nawe zikitoka utatukuta chini ya aridhi hii ya Rwanda. Wewe ebu ruka salama sawa dada” john akaongeza huku akitania ndani yake ili mradi furaha ilejee ndani ya familia hii.

Jovitha aliiaga familia yake na baada ya Nusu saa alikuwa tayari amepanda ndege. Aliitafuta siti yake namba A25LD/1 ambayo ilikuwa Daraja la Kwanza akakaa huku akisubiri muda na kuiacha aridhi ya Kigali na kuelekea UK kwa masomo. Akiwa amekaa kwenye siti yake ametulia, mara akapita mhudumu akiwa ana Novels akiwagawia wasafiri. Mhudumu huyo alipofika kwenye siti aliyokaa Jovitha akatoa novel ya Harry Potter na kumpatia Jovitha aliyekuwa ameweka simu yake sikioni ni baada ya kupigiwa, akaipokea novel nakuiweka pembeni kwenye siti namba A24LD/1. Siti hii ilionekana haina mtu tangia Jovitha alipokaa hapo.

“hallo”Jovitha aliongea na simu

“hallo, how the day Jov” upande wa pili ukajibu

“Im fine, how you too n who am talking to?” Jovitha akajibu na uku akiuliza kama anaongea nani, kwani ilionekana wazi hakutambua anaongea na nani.

“Aaaaaaaaaah aaah, you’ve forgeten my voice? Just try to think 2 years before” upande wa pili ukaongea, uku ukisikika kwa sauti ambayo Jovitha angeiitambua wazi.

“No, who are you? Jovitha akazuga kwani hakutaka ieleweke kama katambua sauti ni ya nani.

“OK,let leave it. Open your novel page24 and don’t end your call” upande wa pili ukatoa maelekezo.

“Ok” Jane akajibu, akichukua kitabu chake alichopewa na kukifungua ukurasa alioelekezwa, alipofanikiwa kuupata ukurasa alishituka sana kwa alichokiona.

“Good by Jov, we shall meet again underworld sorry!!!!!!!!” upande wa pili ukamalizia na simu kukatwa.

“Tafadhali kila mmoja akae kwenye siti na kufunga simu zenu” ilikuwa sauti ya mhudumu mmoja kwenye ndege ikiwa ni ishara ya ndege kuacha aridhi ya Kigali.

Jovitha akiwa amedua kwa muda kwa kile alichokiona, hakuamini macho yake. Mara ghafla jasho jingi kama mfereji wa maji yakamtoka. Akanyanyuka kwenye siti kwa lengo kupata maji ili aweze kunawa uso wake uliojaa jasho kwa kipindi kifupi tu, lakini aliponyanyua hatua mbili za miguu yake akaanguka chini huku akiwa na povu jingi mdomoni likiambatana na damu ambayo ilianza kutoka puani.

“Hallo kapteini tunaomba ndege irudishe kuna tatizo kidogo” mawasiliano yakapelekwa kwa kapiteni wa ndege hiyo.

“Tatizo gani?” kapiteni akauliza.

“kuna mwana dada kaanguka huku daraja la kwanza” mhudumu huyo wa ndege akajibu.

“sawa”kapiteni akakubali kurudisha ndege, kwa kuwa ilikuwa bado kuacha aridhi,

Na hiyo ilikuwa ni baada ya kutoa taarifa kwa waongozaji wa ndege.

“Mmmmh nani tena huyu?” mmoja wa abiria akasikika akiuliza swali. Wakati huo Jovitha akiwa anagalagala chini, hakuwa na uwezo wa kuona zaidi ya kuona kwa shida.

Jovitha” mhudumu mmojawapo akajibu kwa mkato.

“kutoka wapi? Na kwa nini kaanguka mahali hapa?” akaongeza swali lingine ambalo alikupata kujibiwa na yeyote bali watu wote wakageuka na kumuangali muuliza swali tena kwa macho makali, ambapo hadi alipojishitukia mwenyewe kisha kuona haibu na kuondoka eneo hilo.

Jovitha akanyanyuliwa na kuwekwa kwenye machela ambapo alipakiwa kwenye gari la kubebea wagonjwa na ni baada ya kumpa huduma ya kwanza. Baada ya dakika mbili tu ikaanza safari ya kumpeleka hosipitali ya K Hospital ya Jijini Rwanda.

****************************************************************************

Gari la kubebea wagonjwa lilionekana likiwa kasi likikatisha mitaa ya Kigali Road kuelekea K Hospital likiwa karibu kulifikia Daraja la Dotown Bridge. Gari lilipofika karibu kabisa na Daraja Navjay ambaye alikuwa dereva alishangazwa kuwepo kwa watu walioshikiria Binduki mikononi wakiwa wamekaa kwa mashambulizi. Baada ya dreva kuona dalili hiyo akawaagiza wenzake ili wamlinde mgonjwa wao, Jovitha kwa taabu sana alisikia Dereva akiongea ya kwamba ahakikishiwe ulinzi zaidi.
Dereva alivuta mafuta zaidi kuakikisha anavuka kizingiti icho kwani alitambua hao watu hawana amani kabisa. Kweli alivyofikiria ndivyo ilivyokuwa kwani watu hawa walianza kumimina risasi kuelekea wao na risasi nyingi kumpata dereva huyo lakini hakukata tama kabisa, lengo likiwa kuvuka kizingiti na kwa bahati akavuka.
ITAENDELEA
futilia wiki ijayo

No comments:

LATEST NEWS

Share

Widgets

 

Total Pageviews