Social Icons

Monday 10 September 2012

somalia wapata rais mpya

Bunge la Somalia limemchagua
Hassan Sheikh Mohamud kuwa Rais
mpya wa nchi hiyo.
Kulikuwa na wagombea 22 kwenye
uchaguzi huo, akiwemo Rais
anayeondoka Shariff Sheikh Ahmed
na waziri mkuu Abdiweli Mohamed
Ali.
Hassan Sheikh Mohamud alishindat
kufuatia duru ya tatu ya upigaji kura,
ambapo alikuwa anachuana na Rais
anayeondoka Shariff Sheikh Ahmed.
Katika raundi ya kwanza Sheikh
Ahmed alikuwa amepata ushindi
mwembamba wa kura 64 dhidi ya 60
alizopata Sheikh Mohamud.
Kwa jumla wabunge 271 walipiga
kura.
Katika duru ya mwisho wabunge
wengi waliowaunga mkono
wagombea waliochujwa walimuunga
mkono Sheikh Mohamud , akapata
kura 190 dhidi ya 70 alizopata Rais
anayeondoka.
Hii ni mara ya kwanza kwa uchaguzi
wa Rais kufanyika katika mji mkuu wa
Somalia Mogadishu, tangu
kuondolewa kwa serikali ya kijeshi
mwaka 1991.

No comments:

LATEST NEWS

Share

Widgets

 

Total Pageviews