Social Icons

Tuesday, 7 February 2012

NALO HILI MUHIMU, KUUTAZAMA ULIMWENGU !


  •    BARACK OBAMA, RAIS WA MAREKANI. 
“Kuwa Rais kunamsukuma aone uhitaji wa kusali”- Katika hili tunamhitaji kiongozi mwenye misingi ya dini na mwenye kuamini.

  • ·        LA NACION, ARGENTINA
“Walipoulizwa wachague njia ya kuonyesha uzalendo wao, asilimia 56 ya waargentina wenye umri wa kati ya miaka 10 na 24 walisema kwamba wangependa kuvalia jezi ya timu ya kandanda ya Taifa”.-. Hapa kuna jambo la msingi tunaweza kujifunza watanzania. Je sisi kama wazalendo watimu yetu ya Taifa, hili kwetu tumekuwa waraibu tuko tayari kuvaa jezi ya Brazil nakuacha jezi zetu.

  • ·        SHIRIKA LA CHAKULA NA KILIMO LA UMOJA WA MATAIFA, ITALIA.
Matokeo ya utafiti Fulani yalidokeza kwamba “inakadiriwa kwamba asilimia 33 ya chakula kinachozalishwa ulimwenguni pote kwa ajili ya wanadamu hupotea au kutupwa, na hiyo ni kama jumla ya tani bilioni 1.3 kwa mwaka”

  • ·        PATRIARRCH KRILL, MKUU WA KANISA LA OTHODOKSI LA URUSI.
Siku hizi, vita na ripoti za vita zimeenea ulimwenguni pote kwa mfano Misri, Libya Somalia n.k, kwa hiyo jeshi la nchi yetu lazima liwe tayari siku zote kuwalinda watu wake na kila kitu ambacho tunaona kuwa ni kitakatifu kutokana na maadui wanaotoka nchi nyingine.

  • ·        PRESSEPORTAL, UJERUMANI.
Kiwango cha juu cha kabisa aksidenti za magari kilichoripotiwa kwa kampuni moja ya bima nchini ujerumani katika mwaka wa 2010, kilionesha kwamba aksidenti hizo zilitokea kati ya saa mbili asubuhi. “Mojawapo ya njia muhimu zaidi ya kuzuuia aksidenti ni kuwa na wakati wa kutosha wa kusafiri unapoelekea kazini asubuhi,” anasema afisa wa kampuni hiyo.

Saturday, 4 February 2012

Wabunge wazuiwa kujadili mgomo wa madaktari

WABUNGE leo wamezuiwa kujadili kauli ya Serikali kuhusu namna ilivyoshughulikia mgomo wa madaktari.

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, amewaeleza wabunge kuwa, si busara kuijadili kauli hiyo kwa kuwa wamesikia upande mmoja tu wa Serikali, hawajasikia upande wa madaktari wanasema nini.

Ndugia amekiri kwamba suala ni nyeti kwa kuwa linahusu maisha na uhai wa wananchi wanaohitaji tiba lakini taratibu za uendeshaji wa mabunge ya Jumuiya ya Madola haziruhusu kujadili kauli za mawaziri mara tu baada ya kuwasilishwa.

Amesema kutojadili kauli hizo moja kwa moja kunaepusha kauli tofauti tofauti.

Kwa mujibu wa Ndugai, si busara kwa wabunge kuijadili kauli ya Serikali iliyowasilishwa leo bungeni na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda.

Ndugai amesema , madaktari hawajasikilizwa na hawawezi kwenda bungeni kutoa kauli yao lakini licha ya madai mengine, wanawatuhumu watendaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii hawawajibiki na wanatoa kauli za kashfa hivyo si busara kwa wabunge kulijadili suala hilo.

“Sijui kama tutakuwa tunajitendea haki hata sisi wenyewe unless ( isipokuwa) kama tupo informed (kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu jambo fulani” amesema Ndugai.

Ametoa msimamo huo wakati anatoa mwongozo wake kuhusu hoja ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) ya kuomba Bunge lijadili kauli ya Serikali kuhusu namna ilivyoshughulikia mgomo wa madaktari.
Mnyika amesema, ni busara kwa wabunge kuijadili kauli hiyo kwa kuwa, Serikali ni moja ya pande zinazohusika kwenye mgororo huo,hivyo ni busara kauli iliyotoa ijadiliwe na wahusika wawajibishwe.
Mbunge huyo aliomba mwongozo huo kabla Waziri Mponda hajawasilisha kauli hiyo, na baada ya kuwasilishwa, Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR- Mageuzi), na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema) nao waliomba kauli ya Serikali ijadiliwe. Baada ya Ndugai kutoa mwongozo huo aliiagiza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii izungumze na Serikali na madaktari ili kumaliza mgogoro huo.

Ameitaka kamati hiyo hiyo ifanye kazi hiyo haraka na itoe taarifa kuhusu yaliyojiri kwenye mazungumzo hayo na ushauri wa Bunge kwa pande husika.
Amesema, ushauri wa Bunge kwa pande hizo si lazima yawe maagizo, na kwamba, wabunge wanaruhusiwa kuhudhuria vikao vya kamati na pande husika, na kuchangia.

Friday, 3 February 2012

CRDB yaipa Minaki milioni 5/-.

 BENKI ya CRDB imekabidhi sh milioni 5, kwa Shule ya Sekondari ya Minaki ili zitumike kwa ajili ya kuendeleza elimu shuleni hapo. Msaada huo ulitolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dorah Ngarija, wakati wa mahafali ya 52 ya shule hiyo, akisema kiasi hicho kimetolewa kwa lengo la kutatua baadhi ya kero zinazoikabili shule hiyo.

Alisema benki hiyo imekuwa ikitoa mchango mkubwa kwa sekta ya elimu, ikiwemo ya kutoa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ili kupata uzoefu wa kikazi.
Dorah alisema CRDB imefanikiwa kuwapelekea huduma za kibenki wanafunzi wa elimu ya juu ili waendelee kupata huduma za fedha wakiwa vyuoni.

Aliutaka uongozi wa shule hiyo kuendeleza historia iliyoachwa ya kuwa chanzo cha kutoa wanafunzi ambao baadaye watakuwa viongozi bora wa baadaye. Awali, mkuu wa shule hiyo, Arnold Chungu, alisema licha ya shule hiyo kuwa kongwe inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama uhaba wa vifaa, maji safi na salama ya kunywa.

Source: Tanzania Daima

Thursday, 2 February 2012

Madini ya chuma yaleta maafa Nigeria

Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limesema kuwa shughuli ya uchimbaji dhahabu kaskazini mwa Nigeria imewasababishia maelfu ya watoto maradhi mabaya zaidi kutokana na uchafuzi wa madini ya chuma.

Human Rights Watch inasema kuwa uchafuzi huo ndio mbaya zaidi kuwahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni na watoto wengi katika eneo hilo wanahitaji msaada wa kimatibabu. Shirika hilo linasema tayari watoto mia nne wamekwishaaga dunia kutokana na mkasa huo. Baadhi ya watoto hao ambao wana umri wa miaka minane wanafanya kazi katika migodi ya dhahabu katika jimbo la Zamfara.

Viwango vya uchafuzi wa madini ya chuma ni vya juu zaidi katika baadhi ya vijiji na takriban asilimia arobaini ya watoto walioenekana kuwa na dalili ya kupata maradhi yanayotokana na uchafuzi huo wameaga dunia. Shirika la Human Rights Watch linasema kuwa uchimbaji wa madini unawaweka watoto hao katika hatari ya kuathirika na vumbi ya madini hayo ya chuma ambayo inachafua maji pamoja na chakula. Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa madini ya chuma husababisha matatizo ya kudumaa ubongo na umbo la watoto.Read More

Wednesday, 1 February 2012

MWAKYEMBE:”NAMSHUKURU MUNGU KWA KUENDELEA KUNIPA NGUVU”

Kwa muda sasa,hali ya afya ya Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya,Dr.Harrison Mwakyembe, imekuwa ni gumzo lisiloisha.Yanasemwa mengi kuhusu ugonjwa unaomsumbua.Yeye mwenyewe hajaweka bayana juu ya ugonjwa wake.Serikali nayo,kwa kuzingatia taratibu za kitabibu,haiwezi kusema kitu.Bado anaugua.
Pamoja na kwamba bado anaugua,hali yake inaendelea vizuri.Mwishoni mwa wiki alithibitisha hilo pale alipoweza kuhudhuria ibada katika Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mch.Josephat Gwajima lililopo maeneo ya Kawe jijini Dar-es-salaam.

Anavyoonekana hivi sasa Dr.Harrison Mwakyembe



LATEST NEWS

Share

Widgets

 

Total Pageviews