Social Icons

Friday 3 February 2012

CRDB yaipa Minaki milioni 5/-.

 BENKI ya CRDB imekabidhi sh milioni 5, kwa Shule ya Sekondari ya Minaki ili zitumike kwa ajili ya kuendeleza elimu shuleni hapo. Msaada huo ulitolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dorah Ngarija, wakati wa mahafali ya 52 ya shule hiyo, akisema kiasi hicho kimetolewa kwa lengo la kutatua baadhi ya kero zinazoikabili shule hiyo.

Alisema benki hiyo imekuwa ikitoa mchango mkubwa kwa sekta ya elimu, ikiwemo ya kutoa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ili kupata uzoefu wa kikazi.
Dorah alisema CRDB imefanikiwa kuwapelekea huduma za kibenki wanafunzi wa elimu ya juu ili waendelee kupata huduma za fedha wakiwa vyuoni.

Aliutaka uongozi wa shule hiyo kuendeleza historia iliyoachwa ya kuwa chanzo cha kutoa wanafunzi ambao baadaye watakuwa viongozi bora wa baadaye. Awali, mkuu wa shule hiyo, Arnold Chungu, alisema licha ya shule hiyo kuwa kongwe inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama uhaba wa vifaa, maji safi na salama ya kunywa.

Source: Tanzania Daima

No comments:

LATEST NEWS

Share

Widgets

 

Total Pageviews