Social Icons

Friday, 30 March 2012

MAMBO YA ARUMERU HAYO

 Hapa CCM na msafara wao huko Arumeru

 
  
Hapo juu Wanakijiji wakiikaribisha helkopita ianyotumiwa na CHADEMA ilipokuwa ikitua eneo la mkutano Ambureni
 
 Watoto nao hawako mbaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii na hizi kampeni, yaani nipata shika tu Arumeru

Saturday, 24 March 2012

CHADEMA YACHEZEWA RAFU ARUMERU

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa jana alilalamikia kile alichodai kuwa ni kuchezewa mchezo mchafu na makada wa CCM.

Malalamiko ya Dk Slaa yanatokana na kusambazwa barua yenye nembo ya Chadema ambayo ina maneno ya kashfa dhidi ya Meneja Mwenza wa kampeni wa chama hicho, Vincent Nyerere.

Akizungumza kwenye mikutano ya hadhara katika Vijiji vya Nkoanekoli, Kata ya Nkoaranga, Kikwe na Akheri, Dk Slaa alisema amesikitishwa na barua hiyo iliyosambazwa usiku wa manane maeneo ya Tengeru na Leganga.

“Barua hii inaonyesha kama imeandikwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe lakini cha ajabu jina langu limekosewa limeandikwa Silaha wakati siitwi hivyo na imeghushiwa nembo na kumbukumbu ya chama changu. Huu ni wizi ambao haukubaliki hata kisheria,” alisema Dk Slaa.

Akinukuu barua hiyo, Dk Slaa alisema maneno yake yanamshauri kuachana na Vicent Nyerere kwa sababu amemchafua Mkapa, anayeheshimika Meru na nchi nzima, hivyo hali hiyo itasababisha kukosa kura Meru.

“Sisi tumechukua barua hizi na nakala tumepeleka polisi na namtaka Isaya Mngulu amtafute mhusika wa barua hii ili ashughulikiwe kwa sababu kughushi nembo ni kosa kisheria na njia za kumpata ni rahisi sababu anatafutwa hata kwa njia ya kompyuta,” alisema.

Dk Slaa alisema kuwa ugomvi wake siyo kukosewa jina lake wala kumchafua Nyerere, sababu watake wasitake Nyerere ni mtoto wa baba mkubwa wa marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, hivyo hakuna uhusiano na uchaguzi huo.

Alisema ugomvi wake ni kughushi nembo hiyo ya chama na amegundua imeghushiwa baada ya kuwasiliana na Zitto ambaye alikana kuandika barua hiyo wala kuifahamu.

Zitto akizungumza kwenye mkutano wa hadhara jana pia alikana kuitambua barua hiyo.

CCM YA GAWANYWA NA LOWASSA HUKO ARUMERU

USHIRIKI wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge Arumeru Mashariki unadaiwa kuigawa timu ya kampeni ya CCM inayomnadi mgombea wa chama hicho, Sioi Sumari.Lowassa ambaye yuko mkoani Arusha tangu Machi 20, mwaka huu, amekuwa akitajwa kwamba atamnadi Sioi lakini tofauti na makada wengine, hadi sasa hakuna ratiba yoyote ndani ya CCM inayoonyesha ni lini mbunge huyo wa Monduli atapanda jukwaani.

Habari zilizopatikana jana kutoka Arumeru na Dar es Salaam zinasema baadhi ya viongozi wa CCM na timu inayoongoza kampeni za uchaguzi huo wamegawanyika kuhusu Lowassa kupanda jukwaani, huku wengine wakipinga.

Kumekuwepo na kundi ambalo linaona kwamba Lowassa akiingia kwenye kampeni hizo anaweza kuzua mazingira ambayo yataipa ugumu CCM kushinda kutokana na kumbukumbu kuwa alijiuzulu kutokana na kashfa ya utoaji wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura iliyotolewa kwa kampuni tata ya Richmond Development LCC.

Chadema tayari kimetangaza kuwa endapo Lowassa atajitokeza kwenye kampeni hizo kumnadi mgombea wa CCM, watamuumbua kwa kile wanachodai wataweka hadharani tuhuma kinazodai zinamhusu.

Jana, mmoja wa viongozi wa chama hicho alisema: “Hatapanda jukwaani (Lowassa), wala hatothubutu kufanya hivyo kwani tayari ameambiwa aache na huyo aliyemwambia nadhani anamsikiliza, hawezi kukiuka.”

Kauli ya kiongozi huyo inafanana na ile iliyotolewa na mmoja wa makada wakongwe wa CCM anayeshiriki kampeni za Arumeru Mashariki ambaye Machi 20 mwaka huu akiwa Usa River alsikika akisema: "Lowassa hana umuhimu wowote” kwenye kampeni hizo.

Kiongozi huyo alikuwa akichangia mjadala usio rasmi uliokuwa ukiwahusisha makada kadhaa wakongwe wa CCM, walipokuwa wakisubiri kuanza kwa msafara wa kwenda kwenye moja ya mikutano ya kampeni.

Monday, 19 March 2012

DK. HARRISON MWAKYEMBE ARIPOTI OFISINI NA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO


Nauibu Waziri wa Ujenzi Dr Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ofisini kwake kuhusiana na maendeleo ya Afya yake nakusema kwamba yeye sasa yuko fiti kiafya, na ameripoti ofisini rasmi leo hii alipoulizwa maswali kutoka kwa waandishi wa habari akasema mambo yote anaichia serikali kupitia tume maalumu iliyoundwa kufutilia suala la ugonjwa wake

Sunday, 18 March 2012

MWENYEKITI WA CCM KATA YA MBUGUNI AHAMIA CHADEMA

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa CCM wa Serikali ya Kitongoji cha Madukani, eneo la Msitu wa Mbogo, Kata ya Mbuguni,Godzed Minja, juzi amerudisha kadi ya CCM na kujiunga na CHADEMA, wakati makada wa chama hicho wakimnadi Mgombea wao Nassari wilayani humo.


Akizungumza mara baada ya kujiunga na CHADEMA, Mwenyekiti huyo Minja, alisema kuwa amefanya uamuzi huo kutokana na kuona CCM haina sera zaidi ya kusambaza matusi na kashfa badala ya kujibu hoja za msingi.



“Mimi naahidi nitakuwa mwana Chadema safi na mwaminifu na sitarudi nyuma katika mapambano haya, CCM imepoteza mwelekeo,’’ alisema Minja.



Alisema kuwa atatumia muda wake mwingi kuhakikisha CCM katika Kata ya Mbuguni inapotea kabisa kwa sababu hawana sera za kuwaeleza wananchi juu ya ugumu wa maisha waliyosababisha na kuchangia viongozi wa chama hicho kupata wakati mgumu kwa Wananchi.



Naye Mchungaji Israel Natse, akizungumza wakati akimnadi Mgombea wao, Nassari alisema kuwa eneo la Msitu wa Mbogo, Kata ya Mbuguni CCM imekwisha kwa sababu wanachama wengi wamehama chama hicho na kujiungana Chadema, kutokana na sera zao za matusi mbele ya watoto wadogo.



Alisema kuwa wanachama zaidi ya 300 wanasubiri Katibu wa chama hicho Taifa Dk. Slaa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, ili wakabidhi kadi hizo na kukabidhiwa kadi za Chadema mbele yao.



PIA Chadema yataka mdahalo huko Arumeru
Katika hatua nyingine Chadema, kimeomba kufanyika mdahalo wa wagombea wote wa ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ili kutoa fursa kubwa kwa wapigakura wa jimbo hilo na Watanzania kwa ujumla, kuwafahamu.



Meneja Mwenza wa kampeni wa Chadema, Vincent Nyerere, alitoa ombi hilo jana katika mikutano ya kampeni ya chama hicho, katika Kijiji cha Kikatiti na Maleu, wakati mgombea ubunge wa chama hicho, Nassari akiomba kura.



Nyerere ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, alisema uchaguzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki unasura ya kitaifa, hivyo ni busara kutoa fursa kwa Watanzania wengi kuwajua wagombea, sera zao na nini wamejipanga kuwafanyia wakazi wa jimbo hilo.



“Sisi Chadema tunataka wagombea wengine wakubali hasa CCM ambao wamekuwa wakikacha midahalo ili tutowe fursa kwa Watanzania kuwajua wagombea wao kwani kipindi cha kampeni ni kifupi sana, hivyo hakitowi nafasi wagombea kujulikana,”alisema Nyerere.



Awali Nassari aliwataka wakazi wa jimbo hilo kubadilisha siku ya kimataifa ya wajinga ambayo huadhimishwa Aprili mosi kila mwaka kuwa siku ya werevu kwa kuchagua kupinga maisha magumu, kupinga vitu kupanda bei na kupinga Meru kukosa ardhi na maji.



Nassari alisema, kumchagua yeye ni kuondoa shida na mateso yao yanayowakabili kutokana na serikali ya CCM kushindwa kutatua shida zao kwa miaka 50 sasa.



Mgombea huyo, aliendelea kusisitiza kuwa kati yawagombea wote, yeye ndiye anaishi Arumeru na ni mpiga kura wa jimbo hilo, hivyo anajua matatizo ya wakazi wa jimbo hilo.



“Mimi mimezaliwa Meru,nimesoma Meru,naishi Meru na ninafanya kazi Meru hivyo najua matatizo yenu na namna ya kuyatatua”alisema Nassari.




LATEST NEWS

Share

Widgets

 

Total Pageviews