Social Icons

Saturday 24 March 2012

CHADEMA YACHEZEWA RAFU ARUMERU

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa jana alilalamikia kile alichodai kuwa ni kuchezewa mchezo mchafu na makada wa CCM.

Malalamiko ya Dk Slaa yanatokana na kusambazwa barua yenye nembo ya Chadema ambayo ina maneno ya kashfa dhidi ya Meneja Mwenza wa kampeni wa chama hicho, Vincent Nyerere.

Akizungumza kwenye mikutano ya hadhara katika Vijiji vya Nkoanekoli, Kata ya Nkoaranga, Kikwe na Akheri, Dk Slaa alisema amesikitishwa na barua hiyo iliyosambazwa usiku wa manane maeneo ya Tengeru na Leganga.

“Barua hii inaonyesha kama imeandikwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe lakini cha ajabu jina langu limekosewa limeandikwa Silaha wakati siitwi hivyo na imeghushiwa nembo na kumbukumbu ya chama changu. Huu ni wizi ambao haukubaliki hata kisheria,” alisema Dk Slaa.

Akinukuu barua hiyo, Dk Slaa alisema maneno yake yanamshauri kuachana na Vicent Nyerere kwa sababu amemchafua Mkapa, anayeheshimika Meru na nchi nzima, hivyo hali hiyo itasababisha kukosa kura Meru.

“Sisi tumechukua barua hizi na nakala tumepeleka polisi na namtaka Isaya Mngulu amtafute mhusika wa barua hii ili ashughulikiwe kwa sababu kughushi nembo ni kosa kisheria na njia za kumpata ni rahisi sababu anatafutwa hata kwa njia ya kompyuta,” alisema.

Dk Slaa alisema kuwa ugomvi wake siyo kukosewa jina lake wala kumchafua Nyerere, sababu watake wasitake Nyerere ni mtoto wa baba mkubwa wa marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, hivyo hakuna uhusiano na uchaguzi huo.

Alisema ugomvi wake ni kughushi nembo hiyo ya chama na amegundua imeghushiwa baada ya kuwasiliana na Zitto ambaye alikana kuandika barua hiyo wala kuifahamu.

Zitto akizungumza kwenye mkutano wa hadhara jana pia alikana kuitambua barua hiyo.

No comments:

LATEST NEWS

Share

Widgets

 

Total Pageviews