Social Icons

Tuesday 27 November 2012

KIFO CHA SHARO MILIONEA NI PIGO JINGINE 2012

Usiku wa jana ni ulikuwa usiku wa majonzi kwa watanzania wote hasa kwa waliokuwa mashabiki wakubwa wa msanii na mchekeshaji maarufu nchini Sharo Milionea,ambae amefariki dunia kwa ajali mbaya ya gari wakati akitoka Dar es Salaam kueleka wilayani Muheza, Tanga Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Costantine Massawe Hussein Ramadhani (Sharo Milionea) alikuwa akiendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier. Alipofika maeneo ya Segera gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa, likagonga mti nakusababisha kifo chake na yeye kutokea mbele ya kioo cha gari na kutupwa mbali.

Alisema Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza Aliongeza kuwa hakuna kona kali wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali. Gari lake imehifadhiwa mahali salama kwakuwa limeharibika vibaya na kwamba kwenye gari alikuwa mwenyewe.

Habari kuhusu kuthibitika kwa kifo chake zilianza kuenea jana usiku ambapo kwa upande wa rafiki yake
wa karibu Kitale amesema alikuwa
akiipiga simu ya Sharo Milionea iliyokuwa ikiita kwa muda mrefu bila kupokelewa na kisha kupigiwa simu na Tundaman, Mzee Majuto na Mjomba wake Sharokumtaarifu juu ya kifo hicho. Naye Raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bwana Simon Mwakifwamba alisema kwamba “Sisi binadamu tunaweza kuwaza hivi na Mungu naye akawaza lake kwahiyo sisi tunaziombea familia hizi Mungu azipe faraja ya kweli na nadhaniinatoka kwa Mungu,” alisema hayo kwenye kituo cha televisheni ya TBC.

Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wamesema kuwa kifo cha Sharo Milionea kimetokea wakati ambao alikuwa ameanza kufanikiwa “Sharo umri wake na mambo aliyoanza kuyafanya ni makubwa. “Sharo alishaanza kupata matumaini yaani ni sawa sawa unatupa mbegu halafu uitegemee inaanza kuchepua Sharo alishaanza kuchepua,anachepua ile mbegu yake, ameanza kujisaidia yeye kama yeye sababu katika maisha lazima kwanza uanze kujisaidia wewe kama wewe halafu pili uingalie jamii inahitaji nini kwako. Amejipatia usafiri maskini ya Mungu, pa kulala, na maisha yote ya kutoka Dar es Salaam kwenda Tanga kuwaona wazazi kutumia gharama yake.”Maneno hayo yalisemwa na Bwana Steve Nyerere,na pia aliongeza na kusema kuwa Jmbo la msingi ni Kumwachia Mungu na kuondoa mawazo kuhusiana na kifo chake. Umoja wa wasanii wa filamu nchini umesema umepata pigo kubwa sana hasa kwakuwa bado wana msiba wa msanii mwingine wa filamu Marehemu John Stephano ambaye anatarajia kuzikwa leo. Wamesema baada ya mazishi hayo kesho wanatarajia kusafiri na mabasi mawili kuelekea wilayani Muheza kwaajili ya mazishi ya marehemu Hussein Ramandhani(Sharo Millionea).

No comments:

LATEST NEWS

Share

Widgets

 

Total Pageviews