Social Icons

Monday 21 May 2012

IFM WATETEA UBINGWA WA MKOA KWA KUWACHAPA CBE 4-0

Nahodha wa timu ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM), Charles Evance akipokea kitita cha pesa Shilingi Laki tano kutoka kwa Ofisa Utamaduni wa Wilaya ya Kinondoni, Jumanne Mlimi maaara baada ya kuibuka washindi wa kwanza wakati mashindano ya Pool Safari Higher Learning yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya ushindi wa kwanza Shilingi laki tano kutoka kwa kwa Ofisa Utamaduni wa Wilaya ya Kinondoni, Jumanne Mlimi maaara baada ya kuibuka washindi wa kwanza wakati mashindano ya Pool Safari Higher Learning yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam


IFM MABINGWA SAFARI HIGHER LEARNING DAR
CHUO cha usimamizi wa Fedha cha Dar es Salaam(IFM) wametetea ubingwa wao juzi katika mashindano ya Pool Safari Lager Higher Learning yaliyomalizika kwenye Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.
IFM waliutwaa ubingwa huo kwa kuwachapa majirani zao chuo cha Elimu ya Biashara(CBE) 4-0,hivyo kujitwalia tena ubingwa kwa mara ya pili kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kuibuka na zawadi ya kitita cha Shilingi laki tano
Mshindi wa pili katika mashindano hayo ni CBE ambao walizawadiwa laki tatu,wapili ni Chuo cha Ardhi ambao walipata laki mbili na wanne ni Chuo cha DIT ambao walipata laki moja.
Wachezaji wa singles(mmoja mmoja) wanaume alishinda Peter Patrick kutoka chuo cha IFM alinyakua ubingwa akifuatiwa na Goodhope Mamkwe kutoka IFM pia,wakati upande wa Wanawake bingwa alikuwa Modesta David kutoka IFM akifuatiwa na Lilian Meiri kutoka chuo cha CBE.

Mshindi wa kwanza wa singles (mmoja mmoja) wanaume, Peter Patrick akionyesha zawadi yake mara baada ya kukabidhiwa na Ofisa Utamaduni wa Wilaya ya Kinondoni, Jumanne Mlimi mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza wakati mashindano ya Pool Safari Higher Learning yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa kwanza wa singles (mmoja mmoja) wanwake, Modesta David akipokea zawadi yake kutokan kwa Ofisa Utamaduni wa Wilaya ya Kinondoni, Jumanne Mlimi mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza wakati mashindano ya Pool Safari Higher Learning yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Msindi wa kwanza wa singles (mmoja mmoja) wanawake, Modesta David akionyesha zawadi yake kwa furaha mara baada ya kuibuka mshindi wakati wa mashindano hayo ya Pool Safari Higher Learning yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
VYUO 8 VYA ELIMU YA JUU USO VYAFUZU KUSHIRIKI FAINALI ZA SAFARI POOL.
VYUO vinane vimefaulu kuingia katika fainali za mashindano ya Pool Safari Higher Learning yatakayofanyika Mkoani Iringa May 26 mwaka huu kutoka katika Mikoa minane.
Akizungumza mratibu wa mashindano hayo, Michael Machellah vyuo vilivyofaulu kuingia katika fainali hizo ni Morogoro ni Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kilimanjaro ni Chuo cha Ushirika Moshi(MUCCOBS), Dodoma ni St.John,Arusha ni Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Mwanza ni St.Augustine,Iringa ni Ruaha(RUCO),Mbeya ni Chuo cha Uhasibu(TAA) na Dar es Salaam ni Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Wachezaji wa singles(mmoja mmoja) wanaume na wanawake kila mkoa watawakilishwa na mabingwa wa kila mkoa ambapo Morogoro ni Moyo Hamza kutoka Chuo cha Ardhi na Fotunate Shija kutoka chuo cha SUA,Kilimanjaro ni Alphael Jackson kutoka MUCCOBS na Suche Anastasia kutoka KCMUCO ,Dodoma ni justace Mhando kutoka MIPANGO na Lemi Jackson kutoka U-DOM na Waku ,Arusha ni Vicent Katiyega kutoka chuo kikuu cha Arusha(UOA) na Violeth Silas kutoka IAA ,Iringa ni Said Mohamed kutoka RUCO na Beatrice kutoka RUCO, Mwanza ni Joachim Mushi kutoka CBE na Agnes Mtalika wa chuo cha Bugando,Mbeya ni na Dar es Salaam ni Feter Patrick kutoka chuo cha IFM na Modesta David kutoka IFM.

RAIS KIKWETE ATEUA MAJAJI MAHAKAMA YA RUFANI


<><><>  
RAIS KIKWETE
































Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.
Taarifa iliyotolewa jioni hii na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imewataja walioteuliwa ni Jaji Semistodes S. Kaijage na Jaji Kipenka M. Musa.
"Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Mei 21, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi wao ulianza tokea Machi 15, mwaka huu, 2012", taarifa hiyo ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, imesema kabla ya kuteuliwa kwake kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kaijage (57) alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam tangu Mei 17, 2007. Aliteuliwa kuwa Jaji Mahakama Kuu Novemba 28, mwaka 2000.

Naye Jaji Musa (57) alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Pia amewahi kuwa Wakili wa Serikali, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba. Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Septemba 13, 2004.

Sunday 13 May 2012

WANANCHI WA MPOKEA KWA SHANGWE FILIKUNJOMBE



Picha zimepigwa na mdau wa Mjengwablog aliyekuwepo Ludewa kwenye mapokezi ya Mbunge Deo Filikunjombe.

SIMBA YATOLEWA MAPAMBANONI

Katika kipindi cha dakika 90 Simba imefungwa magoli matatu wakati yenyewe haijapata kitu, mchezo huo ulianza saa mbili kamili kwa majira ya Tanzania. Baada ya kuamriwa kupigwa penati kwa kanuni za mashindano hayo.  Timu ya Al Ahly Shandy imeshinda penati 9-8 dhindi timu ya Simba na kuisukumiza nje ya mashindano.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam Simba ilishinda magoli 3-0 na kujiweka katika nafasi nzuri ili kusonga mbele katika michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho inayoandaliwa na Shirikisho la vyama vya mpira wa miguu Afrka (CAF) vizur. Hata hivyo imeshindwa kulinda ushindi wake mnono ilioupata jijini Dar es salaam na kukubali kipigo hicho kilichowasukumiza nje ya mashindano hayo. Chanzo: Fullshangweblog

POLENI SIMBA (RUDI NYUMBANI BILA MTOTO ACHA UARABUNI)

LAKINI ENDELEENI KUWA NA FURAHA KAMA AWALI HILI KULINUSULU TAIFA

MANCHESTER CITY HISTORIA ENGLAND

 

QPR walikokuwa wakicheza pungufu uwanjani wameipa mwanya Man city kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England baada ya kuwa na kiu nao toka mwaka 1968, Dakika ya 48 Joey Barton alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Carlos Tevez hivyo kuipa City nafasi kubwa ya ushindi. Goli la kwanza la City liliwekwa kimiani na Pablo Zabaleta kunako dakika ya 39 lakini Djibril Cisse aliisawazishia QPR dakika ya 48 huku goli la pili la QPR likifungwa na Jamie Mackie na kuifanya
City kuhaha
uwanja mzima kutafuta magoli, Lakini bila ya kutarajia kunako dakika za majeruhi Edin Dzeko akasawazisha dakika ya 90 na Sergio Aguero akapiga la ushindi dakika ya sekunde chache baadaye.

Saturday 12 May 2012

UONGOZI WA UDOM WAENDELEA KUWEKA MSISIMAMO JUU YA MAVAZI KWA WANAFUNZI


Hii ni picha ambazo zinonyesha aina ya mavazi na staili za nywele ambazo Uongozi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma umezipiga marufuku Chuoni Hapo.Na Waraka Huu wa Pili Umetolewa na Kubandikwa leo katika muendelezo wa Kutoa waraka wa mavazi ambao wa kwanza ulibandikwa jana

MBIO ZA MWENGE ZANDULIWA MBEYA JANA

Wananchi na Viongozi mbalimbali wakishuhudia shughuli za kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru leo jijini Mbeya.

Vijana wa kundi la halaiki kutoka katika shule mbalimbali za mkoa wa Mbeya wakipamba shughuli za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2012 zinazoongozwa na kauli mbiu ya Sensa ya watu na Makazi ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo yetu, Shiriki kuhesabiwa Agosti 26 leo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya .
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati) akiwasha mwenge wa uhuru kuashiria kuanza kwa mbio za mwenge huo kwa mwaka 2012 leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Mwenge huo utakimbizwa kwenye jumla ya Halmashauri za wilaya, Manispaa na miji 157 na kuongozwa na kauli mbiu ya Sensa ya watu na Makazi ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo yetu Shiriki kuhesabiwa Agosti 26.

Thursday 10 May 2012

Yemen: Al-Qaida Hotbed for Terror 101

This week on Around the World, Christiane Amanpour speaks with David Ignatius of the Washington Post to discuss the foiled Al-Qaida terror plot targeting an overseas jetliner and the country of origin of the plot, Yemen.
Yemen is one of the regions poorest countries and al-Qaida has taken advantage of their political unrest to gain influence and set up a home base of operations. This is where bomb builder Ibrahim Al-Asiri has set up shop, working to to construct an undetectable bomb to take down airplanes heading towards the United States.
These developments come a week after the released private papers of Osama Bin Laden, a year after his death. These memos provide unique insight on the inner workings of the much diminished al-Qaida infrastructure. David Ignatius reveals why al-Qaida's current leader Ayman al-Zawahiri is the just the person U.S. officials were hoping would assume leadership of the terror organization.
In the released papers, Ignatius was fascinated to learn that unlike previous homicidal mass-murderers like Stalin or Hitler, Bin Laden was open to advice and criticism from those around him and was willing to admit when he made a mistake.
Bin Laden eventually came to understand that he turned much the public against him and made serious mistakes in allowing al-Qaida affiliates to kill so many Muslims in Iraq and Afghanistan. "I found it fascinating that he was honest enough, self critical enough, to realize what huge mistakes he made."
But while Bin Laden may have made some serious mistakes in alienating Muslims, he was an effective leader, someone who could attract followers and get them to buy into his message.
That's not so for the current leader. U.S. officials told Ignatius that if they could pick someone to lead al-Qaida it would be current leader Ayman al-Zawahiri. They believe he is a divisive figure within the organization and has a hard time rallying al-Qaida's diverse membership. From the released papers we also learn that Bin Laden and al-Zawahiri fought over all kinds of issues including broad strategies and tactics.

MAONI YA WA TANZANIA JUU YA MAGEUZI YA MSISIMAMO WA OBAMA ZIDI YA NDOA YA JINSIA MOJA TOKA MTANDAO WA KIJAMII FACEBOOK

HOJA IMETOLEWA NA Steven Mwakyusa avia mobile "Obama ameunga mkono ushoga huko kwao, cha ajabu wabongo wanahamaki kana kwamba hayo mambo yameamuliwa hapa kwetu. Hivi watz tuna akili gani? Mbona tunashindwa kujiamini?"

Machibya Tungu We unafikiri akitaka kuleta msaada wa NET akasema lazima tukubali utaratibu huo kuna kiongozi gani wa Tz atapinga??
Watz lazima wahamaki kwani wanajua kesho ama keshokutwa haya mambo yanaingia Tz @steven.

Machibya Tungu Yanatuhusu sana kwa namna nilivyosema hapo juu @charles

Steven Mwakyusa Ngalawa umeongea jambo la msingi, ya Ngoswe tumuachie Ngoswe....tuna matatizo mengi sana kama taifa.
 
Junior Mwakagile mmmmmmmmmmmmmmmmmmmh!iz ndo siasa za wenzetu

Gays and lesbians marriages should be the last things to be worried in Tanzania!Nchi ambayo haina hata maji ya kunywa saafi kwa wananchi wake na madawa kwa watoto na akina mama hospitalini,nchi mbayo hadi leo chini na mti wa Nkuyu linageuzw...a darasa la kusomea wanafunzi ndiyo tunaanza leo kuhamaki kuhusu ndoa za jinsia moja tena zikifanyika nchini Marekani?Waziri Mgimwa kwanza imarisha nguvu ya hela yetu dhidi ya Dollar ya Obama ndiyo tuzungumzie haya ya ushoga bana!See More
 
Steven Mwakyusa Machibya unataka kusema tz haiwezi kwenda bila misaada? Hivi unajua kwamba ule msaada aliohaid Bush wa USD 700M ni makusanyo ya kodi ya mwezi mmoja kwa Dar peke yake yakisimamiwa ipasavyo?
 
Andrew Isaac Mwalusako bora tufe maralia @ machibya tungu, kukubaliana utakuwa ni ushenz wa leaders wetu.

Steven Mwakyusa Andrew unataka kusema kwamba hatuwezi kununua vyandarua wenyewe? Toka wameanza kutoa hyo misaada kuna mabadiliko yeyote? Kwanini wasitoe msaada wa kuua mbu?
 
hapana Steven Mwakyusa hujui kuwa hili suala linahusu binadamu mojakwamoja mfano:watu huwa tunaguswa na vita ambavyo vinapiganwa nje ya nchi yetu na mwisho wa siku unakuta vinagusa mifuko yetu sasa katika hili ni lazima tushtuke kwa kuw...a hata hili mwisho wa siku litatuhusu kwa na namna moja ama nyingine kulingana na jinsi tunavyo endeshwa na viongozi/serikali yetu na hata pia watu wetu kwa jinsi wanavyopenda kuiga vitu kutoka nje bila kuchanganua mambo kwa kina.See More
 

Steven Mwakyusa weston kwamba haya mambo yanaanza baada ya Obama kusupport? Mbona mashoga wapo mitaani, lini watanzania walishinikiza sheria itungwe kuwadhibiti? Unafiki mbaya sana, tena hawa wanaohamaki ukichunguza matendo yao ni aibu.
 

Ramadhani Masudi Mwakyusa, hili swala hujalifikiria kiundani. Kiongozi mwenye heshima kubwa kama obama hapaswi kuongea mambo ya kijinga kama hayo. Nchi zinazoendele hupenda kuiga mambo kutoka nchi zilizoendelea!
 

Steven Mwakyusa Ujinga unaupimaje? Najua utasema siyo utamaduni wetu, je utamaduni wetu ni upi? Kuoa mke mmoja na kuwa na nyumba ndogo kibao? Ngono kabla ya ndoa, ulevi na ufisadi?
 

Joseph Weston hapana Steven Mwakyusa lakini kumbuka si kwamba ukiona ubaya ndio unatakiwa kuuhararisha nakupa mfano mwingine je hapa tanzania kuna wauzaunga na sheria zimetungwa kuzuia hii biashara lakini bado ndo inazidi kukua kwahiyo tuhararishe?
 
Steven Mwakyusa Weston tuhararishe, ila sioni mantik ya kuhamaki mambo ya wengine na kuyafanya big deal....kwani hatuna utash wa kutambua mema na mabaya? Vipi tumeshindwa kujisimamia wenyewe
 
Andrew Isaac Mwalusako mi nafikir obama ni rais idiot kupita marais wengine. Mageuzi yake zidi ya n ndoa ya jinsia moja ni upuuzi.

 
Ramadhani Masudi Mwakyusa, tambua kua kama wewe una upeo wa kujisimamia wengine hawana upeo huo. So usijiangalie wewe kwa kua una utambuzi wa kujisimamia kwa maana wengine hawana uelewa huo! Jaribu kua m2 wa wa2 wote.

 
Gwamaka Mwamasage Naweza kuwalaumu au nisiwalaumu watu wanaohofia kukubali kwa Obama b'coz Marekani ndio dunia kwa sasa na huo ndio ukweli so kama rais wa marekani akiridhia jambo kuna uwezekano viongozi we2 wakishinikizwa watalainika Steven au ushawasahau viongozi wetu?

Wednesday 9 May 2012

MAGEUZI YA MSISIMAMO WA OBAMA ZIDI YA NDOA YA JINSIA MOJA

Obama Jumatano tangazo ilikuwa mabadiliko ya mtazamo wake wa 2004 kuwa "ndoa ni kitu kutakaswa kati ya mwanaume na mwanamke." Wakati huo, pia alisema kuwa vyama vya wenyewe kwa wenyewe walikuwa kutosha kwa ajili ya mashoga na wasagaji Yeye uridhike. Kwamba tofauti kati ya ndoa na vya wenyewe kwa wenyewe vyama vya wafanyakazi ni sehemu tu suala la "semantiki."
According to Chicago's Daily Herald, while Obama was running for Senate in early 2004, he told the newspaper's editorial board that the gay rights struggle was comparable to the 1960s civil rights movement, saying that his father and mother wouldn't have been allowed to marry in some Southern states. Kwa mujibu wa Daily Chicago wa Herald, wakati Obama alikuwa akikimbia kwa ajili ya Seneti ya mwanzoni mwa mwaka 2004, aliiambia gazeti la bodi kuwa mashoga haki za mapambano alikuwa kulinganishwa na miaka ya 1960 harakati wa haki za kiraia, akisema kuwa baba na mama yake ingekuwa asiruhusiwe kuoa katika baadhi ya majimbo ya Kusini. "So it's not as if I'm not sympathetic to the idea that … politics shouldn't get in the way if something's right," Obama told the newspaper. "Kwa hiyo si kama nina huruma sana na wazo kwamba siasa ... haipaswi kupata njia ikiwa haki ya kitu," Obama ameliambia gazeti hilo.

BAAADA YA KUPATIKANA KWA KIASI FULANI,SAJUKI SASA KUONDOKA

Msanii wa filamu Juma Kilowoko maarufu kwa jina la Sajuki ambaye anasumbuliwa na maradhi ya uvimbe tumboni kwa muda mrefu sasa anaondoka nchini leo kuelekea India kwa matibabu yake baada ya kusumbuliwa na ugonjwa huo na kukosa matibabu hapa nchini. Safari ya msanii huyo imekuja baada ya wadau wa filamu, wasanii na
watu mbalimbali kujitolea kwa nyakayi tofauti ili kuweza kufanikisha matibabu ya msanii huyo wa siku nyingi ambaye pia ni Director, Jumla ya Tsh. 16 milioni ziliweza kupatikana huku ikiwa bado inahitajika Tsh. 9 milioni ili kukamilisha kiwango kilichokusudiwa kukusanywa kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo, na pia ziliweza kupatikana tiketi tatu za ndege za kwenda na kurudi nchini India.Tunakutakia kila la kheri Sajuki na Mungu akubaliki.

Obama declares support for gay marriage

President Obama today announced that he now supports same-sex marriage, reversing his longstanding opposition amid growing pressure from the Democratic base and even his own vice president.

In an interview with ABC News’ Robin Roberts, the president described his thought process as an “evolution” that led him to this place, based on conversations with his own staff members, openly gay and lesbian service members, and conversations with his wife and own daughters.

"I have to tell you that over the course of several years as I have talked to friends and family and neighbors when I think about members of my own staff who are in incredibly committed monogamous relationships, same-sex relationships, who are raising kids together, when I think about those soldiers or airmen or marines or sailors who are out there fighting on my behalf and yet feel constrained, even now that Don't Ask Don't Tell is gone, because they are not able to commit themselves in a marriage, at a certain point I’ve just concluded that for me personally it is important for me to go ahead and affirm that I think same sex couples should be able to get married,” Obama told Roberts, in an interview to appear on ABC’s “Good Morning America” Thursday. Excerpts of the interview will air tonight on ABC’s “World News with Diane Sawyer.”

The president stressed that this is a personal position, and that he still supports the concept of states deciding the issue on their own. But he said he’s confident that more Americans will grow comfortable with gays and lesbians getting married, citing his own daughters’ comfort with the concept.

“It’s interesting, some of this is also generational,” the president continued. “You know when I go to college campuses, sometimes I talk to college Republicans who think that I have terrible policies on the economy, on foreign policy, but are very clear that when it comes to same sex equality or, you know, believe in equality. They are much more comfortable with it. You know, Malia and Sasha, they have friends whose parents are same-sex couples. There have been times where Michelle and I have been sitting around the dinner table and we’re talking about their friends and their parents and Malia and Sasha, it wouldn’t dawn on them that somehow their friends’ parents would be treated differently

Tuesday 8 May 2012

AIRTEL YASHIRIKI UWEKAJI WA MKONGO WA MAWASILIANO KUTOKA DAR-TANZANIA HADI SHELISHELI

 

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano
Mallya (kushoto) na Meneja Mawasliano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando
wakijibu maswali ya wanahabari wakati wa uzinduzi rasmi wa uwekaji wa
mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania hadi nchini
Seychelles katika eneo la Msasani, jijini humo jana. Airtel ni moja
ya makampuni yanayosimamia mradi huo.
Waziri wa Viwanda na Maliasili wa Seychelles, Peter Sinon
(kushoto), wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya
(wa pili kulia), mafundi na wawakilishi kutoka Seychelees na Tanzania
wakionyesha kipande cha mkongo wa mawasiliano kama ishara ya uzinduzi
wa uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam
Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo la Msasani, jijini humo
jana. Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia mradi huo.



Waziri wa Maliasili na Viwanda wa Shelisheli Bw. Peter Sinon amesema nchi yake itanufaika na upatikanaji wa mawasiliano ya mkongo wa taifa kutoka Tanzania kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya taifa hilo.
Mkongo wa taifa wa mawasiliano uliozinduliwa miaka 2 iliyopita na Rais Jakaya Kikwete umeweza kuzinufaisha nchi jirani kama Kenya, Uganda, Rwanda,Burundi na sasa Shelisheli.
Akiongea katika fukwe za bahari ya hindi jijini Dar es Salaam eneo la msasani ambako uwekaji wa mlongo huo ndio ulikoanzia mwishoni mwa wiki hii Waziri Sinon amesema kuwa mpango huo ukimalika utaiweza nchi yake kukuza sekta ya mawasiliano na upatikanaji wa taarifa mbalimbali jambo litakalo saidia kukuza uchumi wa nchi hiyo.
“Hii ni nafasi nzuri ya kipekee na ndio maana hata sisi shelisheli tunaipa kipaumbele ili kukamilisha zoezi hili la uwekaji wa mkongo huu wa mawasiliano, tunaamini tukimaliza kila kitu itasaidia sana kukuza pato la nchi kulingana na umuhimu wa mawasiliano” alisema Bw Peter Sinon- Waziri wa Maliasili na Viwanda Shelisheli
Kwa uapnde wake Katibu Mkuu kiongozi kwenye ofisi ya makamu wa rais wan chi hiyo anayeshughulikia ICT Bw Benjamin Choppy ameelezea faida za uwepo wa mkongo huo kuwa ni pamoja na kutoa mawasiliano ya uhakika na bora kwa nchi hiyo
“Sasa hii ni dalili ya kutoa bidhaa bora ya mawasiliano kwa kuwa ukamilifu wa uwekaji mkongo huu tutapata mwasiliano bora zaidi” alimaliza kwa kusema Katibu Mkuu kiongozi kwenye ofisi ya makamu wa rais wan chi hiyo anayeshughulikia ICT Bw Benjamin Choppy
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano Mallya ameelezea upatikanaji wa teknolojia hiyo mpya ya mawasiliano kuwa ni kati ya vitu ambavyo Airtel inavifanyia kazi kuhakikisha inaunganisha mataifa mengi ili kutoa mawasiliano yanayotoa nafasi au fulsa ya kuendeleza nchi hizo kijamii na kiuchumi pia
“tunaamini ushirikiano wetu na wenzetu wa shelisheli ni dhahiri utachangia sana kuboresha mahusiano yetu kibiashara na pia kutoa nafasi kwa nchi hizi kujijenga kijamii ma kiuchumu kutokana na faida ya mahusiano haya ya kulaza mkongo huu wa kuunganisha mawasiliano” alisema Bi Beatrice Singano Mallya
Aitel Tanzania na Airtel Shelisheli kwa kushirikiana na SCS zinatekeleza mpango wa kuweka mkongo wa taifa kwa lengo la kuiwezesha nchi hiyo kuwa na mawasiliano ya uhakika.

Mkapa atoa ushahidi mahakamani


Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa afika mahakamani kutoa ushahidi
Rais Mstaafu Tanzania Benjamin William Mkapa amefika mbele ya mahakama akiwa ni shahidi wa kwanza upande wa utetezi katika mashataka yanayomkabili aliyewahi kuwa balozi waTanzania nchini Italia Profesa Costa Mahalu.
Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi aliyewahi kushika madaraka makubwa nchiniTanzaniakufika mbele ya mahakama akitakiwa kutoa ushahidi upande wa utetezi dhidi ya ya tuhuma zinamzomkabili mmoja wa watumishi katika kipindi cha utawala wake.
Katika Mahakama ya hakimu mkazi ya kisutu iliyojaa watu wengi Rais huyo mstaafu mara baada ya kuapa ameieleza mahakama kuwa serikali yake ilifahamu na kisha kuridhia ununuzi wa nyumba au jengo la ubalozi waTanzania nchini Italia baada ya kushauriana na Balozi waTanzanianchini Italia wakati huo Profesa Costa Mahalu.
Hatua hiyo ilifuatia kuthaminiwa kwa jengo lenyewe kulikofanywa na Mamlaka husika kutoka serikali yaTanzania. Baadaye jengohilolilinunuliwa na Bw Mkapa kulizidnua rasmi alipokuwa ziarani kikazi nchini Italia Mwezi February mwaka 2003.
Akijibu swali la wakili upande wa mashtaka ni kwa nini malipo ya shilingi Bilioni mbili na milioni 900 yakafanyika kwa kupitia akaunti mbili tofauti,Bwana Mkapa ameiambia mahakama hiyo kuwa alijulishwa kuwa hilo lilikuwa sharti na muuzaji nyumba na hivyo kwa upande wa serikali hakuona kama kuna tatizo akizingatia kuwa thamani ya jengo iliishafanywa na kuwaridhisha wao kama serikali huku kukiwa na mahitaji makubwa ya Serikali ya Tanzania kuwa na majengo ya kudumu ambayo yangemilikiwa na serikal.
Mmoja wa mawakili ambaye alimuongoza Bwana Makapa kutoa ushahidi wake Wakili Alex Mgongolwa alimweleza mwandishi wa BBC Eric Nampesya mjini Dar es salaam kuwa amefurahia kumuongoza Bwana Mkama kutoa ushahidi wake mahakamani. Alisema ‘kitendo cha Rais mstaafu kufika mahakamani kama shahidi kwa upande mwingine kimeonyesha ni jinsi gani misingi ya sheria inaheshimiwa wakiwemo kiongozi wastaafukamaBwana Benjamin Mkapa.’

Bw Mkapa akiwa na viongozi wengine wa Afrika
Kiongozi huyo anakuwa wa kwanza katika historia yaTanzaniakwa miaka zaidi ya hamsini kwa kiongozi aliyewahi kuwa Rasi kufika mbele ya mahakama na kutoa ushahidi.
Katika kesi hiyo Balozi huyo wa zamani wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa Mahalu anashtakiwa kwa kuhujumu uchumi ambapo inadakiwa kuwa alitoa taarifa za uongo kuhusu bei halisi ya jengo la ubalozi lililonunuliwa na serikali ya Tanzania kwa kutaja bei ya juu, ikiwa ni tofauti na bei yake halisi.
Prof Costa Mahalu anadaiwa kuisababishia serikali ya Tanzania hasara ya $ 3.098 milioni (shilingi bilioni 2 na milioni 900 za Tanzania).

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI OMBI LA LULU

Msanii wa filamu za maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, leo amepandishwa tena kizimbani mara ya tatu katika kesi ya mauaji ya Kanumba inayomkabili ambapo mawakili wanaomtetea wakiongozwa na Kennedy Fungamtama waliwasilisha ombi la kurekebisha umri wa mshitakiwa huyo kuwa miaka 17 na si 18 kama ilivyowasilishwa mahakamani hapo.
Fungamtama na jopo lake walisema mteja wao ni mtoto mdogo hivyo kesi hiyo ipelekwe mahakama ya watoto na kuwasilisha cheti kinachoonesha ana umri wa miaka 17. Upande wa mashitaka umetupilia mbali ombi hilo na kudai cheti kilichowasilishwa kina mapungufu kadhaa likiwemo jina la Dyana ambalo halijawahi kusikika likitumiwa na mshitakiwa huyo

Katika hali ya kustaajabisha!!
IMEBAINIKA kuwa wasanii wawili maarufu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Kajala Masanja ambao sasa wako katika matatizo wakikabiliwa na tuhuma mbili tofauti sasa wamemgeukia Mungu.
Inasemekana kuwa mara baada ya kukutana gerezani na kuombewa na waumini wa Kanisa la Efatha wamekuwa wakishinda wakisoma Biblia.
Habari zinasema licha ya kusoma kitabu hicho kitakatifu kwa waumini wa Kikristo, wasanii hao wamekuwa wakivaa rozali wakati wote badala ya cheni za dhahabu ambazo walikuwa wakivaa walipokuwa uraiani.
“Hivi sasa wamekuwa wakining’iniza rozali shingoni badala ya kuvaa mikufu ya dhahabu, na wamekuwa wakisoma sana Biblia wakiamini kuwa Mungu atawasaidia katika matatizo yao, hakika nakuhakikishia kuwa sasa wamebadilika sana,” kilisema chanzo hicho.

Friday 4 May 2012

ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI

MAWAZIRI

1. OFISI YA RAIS
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)

Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)

Ndugu George Mkuchika, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)

Ndugu Celina Kombani, Mb.,

2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)

Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)

Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,

3. OFISI YA WAZIRI MKUU
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)

Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)

Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)

Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,

4. WIZARA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,

Waziri wa Ujenzi

Dr. John P. Magufuli, Mb.,

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,


 Waziri wa Katiba na Sheria

Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

Dr. David M. David, Mb.,

Waziri wa Kazi na Ajira

Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Prof. Makame M. Mbarawa, Mb.,

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb.,

Waziri wa Maji

Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,

Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum

Prof. Mark Mwandosya, Mb.,

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

Eng. Christopher Chiza, Mb.,

Waziri wa Uchukuzi

Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,

Waziri wa Maliasili na Utalii

Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,

Waziri wa Viwanda na Biashara

Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,

Waziri wa Fedha

Dr. William Mgimwa, Mb.,

Waziri wa Nishati na Madini

Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,

5. NAIBU MAWAZIRI

              OFISI YA RAIS
              HAKUNA NAIBU WAZIRI

 6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais

Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,


7. OFISI YA WAZIRI MKUU
 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)

Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)

Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,

8. WIZARA MBALIMBALI

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira

Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

Ndugu Adam Malima, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara

Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,

Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii

Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,

Naibu Waziri wa Ujenzi

Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,

Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,

Naibu Waziri wa Nishati na Madini

Ndugu George Simbachawene, Mb.,

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Ndugu January Makamba, Mb.,

Naibu Waziri wa Uchukuzi

Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Ndugu Amos Makala, Mb.,

Naibu Waziri wa Maji

Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,

Naibu Waziri Nishati na Madini

Ndugu Stephen Maselle, Mb.,

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria

Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha

Ndugu Janet Mbene, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha

Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.

LATEST NEWS

Share

Widgets

 

Total Pageviews