Social Icons

Thursday 10 May 2012

MAONI YA WA TANZANIA JUU YA MAGEUZI YA MSISIMAMO WA OBAMA ZIDI YA NDOA YA JINSIA MOJA TOKA MTANDAO WA KIJAMII FACEBOOK

HOJA IMETOLEWA NA Steven Mwakyusa avia mobile "Obama ameunga mkono ushoga huko kwao, cha ajabu wabongo wanahamaki kana kwamba hayo mambo yameamuliwa hapa kwetu. Hivi watz tuna akili gani? Mbona tunashindwa kujiamini?"

Machibya Tungu We unafikiri akitaka kuleta msaada wa NET akasema lazima tukubali utaratibu huo kuna kiongozi gani wa Tz atapinga??
Watz lazima wahamaki kwani wanajua kesho ama keshokutwa haya mambo yanaingia Tz @steven.

Machibya Tungu Yanatuhusu sana kwa namna nilivyosema hapo juu @charles

Steven Mwakyusa Ngalawa umeongea jambo la msingi, ya Ngoswe tumuachie Ngoswe....tuna matatizo mengi sana kama taifa.
 
Junior Mwakagile mmmmmmmmmmmmmmmmmmmh!iz ndo siasa za wenzetu

Gays and lesbians marriages should be the last things to be worried in Tanzania!Nchi ambayo haina hata maji ya kunywa saafi kwa wananchi wake na madawa kwa watoto na akina mama hospitalini,nchi mbayo hadi leo chini na mti wa Nkuyu linageuzw...a darasa la kusomea wanafunzi ndiyo tunaanza leo kuhamaki kuhusu ndoa za jinsia moja tena zikifanyika nchini Marekani?Waziri Mgimwa kwanza imarisha nguvu ya hela yetu dhidi ya Dollar ya Obama ndiyo tuzungumzie haya ya ushoga bana!See More
 
Steven Mwakyusa Machibya unataka kusema tz haiwezi kwenda bila misaada? Hivi unajua kwamba ule msaada aliohaid Bush wa USD 700M ni makusanyo ya kodi ya mwezi mmoja kwa Dar peke yake yakisimamiwa ipasavyo?
 
Andrew Isaac Mwalusako bora tufe maralia @ machibya tungu, kukubaliana utakuwa ni ushenz wa leaders wetu.

Steven Mwakyusa Andrew unataka kusema kwamba hatuwezi kununua vyandarua wenyewe? Toka wameanza kutoa hyo misaada kuna mabadiliko yeyote? Kwanini wasitoe msaada wa kuua mbu?
 
hapana Steven Mwakyusa hujui kuwa hili suala linahusu binadamu mojakwamoja mfano:watu huwa tunaguswa na vita ambavyo vinapiganwa nje ya nchi yetu na mwisho wa siku unakuta vinagusa mifuko yetu sasa katika hili ni lazima tushtuke kwa kuw...a hata hili mwisho wa siku litatuhusu kwa na namna moja ama nyingine kulingana na jinsi tunavyo endeshwa na viongozi/serikali yetu na hata pia watu wetu kwa jinsi wanavyopenda kuiga vitu kutoka nje bila kuchanganua mambo kwa kina.See More
 

Steven Mwakyusa weston kwamba haya mambo yanaanza baada ya Obama kusupport? Mbona mashoga wapo mitaani, lini watanzania walishinikiza sheria itungwe kuwadhibiti? Unafiki mbaya sana, tena hawa wanaohamaki ukichunguza matendo yao ni aibu.
 

Ramadhani Masudi Mwakyusa, hili swala hujalifikiria kiundani. Kiongozi mwenye heshima kubwa kama obama hapaswi kuongea mambo ya kijinga kama hayo. Nchi zinazoendele hupenda kuiga mambo kutoka nchi zilizoendelea!
 

Steven Mwakyusa Ujinga unaupimaje? Najua utasema siyo utamaduni wetu, je utamaduni wetu ni upi? Kuoa mke mmoja na kuwa na nyumba ndogo kibao? Ngono kabla ya ndoa, ulevi na ufisadi?
 

Joseph Weston hapana Steven Mwakyusa lakini kumbuka si kwamba ukiona ubaya ndio unatakiwa kuuhararisha nakupa mfano mwingine je hapa tanzania kuna wauzaunga na sheria zimetungwa kuzuia hii biashara lakini bado ndo inazidi kukua kwahiyo tuhararishe?
 
Steven Mwakyusa Weston tuhararishe, ila sioni mantik ya kuhamaki mambo ya wengine na kuyafanya big deal....kwani hatuna utash wa kutambua mema na mabaya? Vipi tumeshindwa kujisimamia wenyewe
 
Andrew Isaac Mwalusako mi nafikir obama ni rais idiot kupita marais wengine. Mageuzi yake zidi ya n ndoa ya jinsia moja ni upuuzi.

 
Ramadhani Masudi Mwakyusa, tambua kua kama wewe una upeo wa kujisimamia wengine hawana upeo huo. So usijiangalie wewe kwa kua una utambuzi wa kujisimamia kwa maana wengine hawana uelewa huo! Jaribu kua m2 wa wa2 wote.

 
Gwamaka Mwamasage Naweza kuwalaumu au nisiwalaumu watu wanaohofia kukubali kwa Obama b'coz Marekani ndio dunia kwa sasa na huo ndio ukweli so kama rais wa marekani akiridhia jambo kuna uwezekano viongozi we2 wakishinikizwa watalainika Steven au ushawasahau viongozi wetu?

No comments:

LATEST NEWS

Share

Widgets

 

Total Pageviews