Social Icons

Friday 30 March 2012

MAMBO YA ARUMERU HAYO

 Hapa CCM na msafara wao huko Arumeru

Hapo juu Wanakijiji wakiikaribisha helkopita ianyotumiwa na CHADEMA ilipokuwa ikitua eneo la mkutano Ambureni
 
 Watoto nao hawako mbaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii na hizi kampeni, yaani nipata shika tu Arumeru

Saturday 24 March 2012

CHADEMA YACHEZEWA RAFU ARUMERU

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa jana alilalamikia kile alichodai kuwa ni kuchezewa mchezo mchafu na makada wa CCM.

Malalamiko ya Dk Slaa yanatokana na kusambazwa barua yenye nembo ya Chadema ambayo ina maneno ya kashfa dhidi ya Meneja Mwenza wa kampeni wa chama hicho, Vincent Nyerere.

Akizungumza kwenye mikutano ya hadhara katika Vijiji vya Nkoanekoli, Kata ya Nkoaranga, Kikwe na Akheri, Dk Slaa alisema amesikitishwa na barua hiyo iliyosambazwa usiku wa manane maeneo ya Tengeru na Leganga.

“Barua hii inaonyesha kama imeandikwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe lakini cha ajabu jina langu limekosewa limeandikwa Silaha wakati siitwi hivyo na imeghushiwa nembo na kumbukumbu ya chama changu. Huu ni wizi ambao haukubaliki hata kisheria,” alisema Dk Slaa.

Akinukuu barua hiyo, Dk Slaa alisema maneno yake yanamshauri kuachana na Vicent Nyerere kwa sababu amemchafua Mkapa, anayeheshimika Meru na nchi nzima, hivyo hali hiyo itasababisha kukosa kura Meru.

“Sisi tumechukua barua hizi na nakala tumepeleka polisi na namtaka Isaya Mngulu amtafute mhusika wa barua hii ili ashughulikiwe kwa sababu kughushi nembo ni kosa kisheria na njia za kumpata ni rahisi sababu anatafutwa hata kwa njia ya kompyuta,” alisema.

Dk Slaa alisema kuwa ugomvi wake siyo kukosewa jina lake wala kumchafua Nyerere, sababu watake wasitake Nyerere ni mtoto wa baba mkubwa wa marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, hivyo hakuna uhusiano na uchaguzi huo.

Alisema ugomvi wake ni kughushi nembo hiyo ya chama na amegundua imeghushiwa baada ya kuwasiliana na Zitto ambaye alikana kuandika barua hiyo wala kuifahamu.

Zitto akizungumza kwenye mkutano wa hadhara jana pia alikana kuitambua barua hiyo.

CCM YA GAWANYWA NA LOWASSA HUKO ARUMERU

USHIRIKI wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge Arumeru Mashariki unadaiwa kuigawa timu ya kampeni ya CCM inayomnadi mgombea wa chama hicho, Sioi Sumari.Lowassa ambaye yuko mkoani Arusha tangu Machi 20, mwaka huu, amekuwa akitajwa kwamba atamnadi Sioi lakini tofauti na makada wengine, hadi sasa hakuna ratiba yoyote ndani ya CCM inayoonyesha ni lini mbunge huyo wa Monduli atapanda jukwaani.

Habari zilizopatikana jana kutoka Arumeru na Dar es Salaam zinasema baadhi ya viongozi wa CCM na timu inayoongoza kampeni za uchaguzi huo wamegawanyika kuhusu Lowassa kupanda jukwaani, huku wengine wakipinga.

Kumekuwepo na kundi ambalo linaona kwamba Lowassa akiingia kwenye kampeni hizo anaweza kuzua mazingira ambayo yataipa ugumu CCM kushinda kutokana na kumbukumbu kuwa alijiuzulu kutokana na kashfa ya utoaji wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura iliyotolewa kwa kampuni tata ya Richmond Development LCC.

Chadema tayari kimetangaza kuwa endapo Lowassa atajitokeza kwenye kampeni hizo kumnadi mgombea wa CCM, watamuumbua kwa kile wanachodai wataweka hadharani tuhuma kinazodai zinamhusu.

Jana, mmoja wa viongozi wa chama hicho alisema: “Hatapanda jukwaani (Lowassa), wala hatothubutu kufanya hivyo kwani tayari ameambiwa aache na huyo aliyemwambia nadhani anamsikiliza, hawezi kukiuka.”

Kauli ya kiongozi huyo inafanana na ile iliyotolewa na mmoja wa makada wakongwe wa CCM anayeshiriki kampeni za Arumeru Mashariki ambaye Machi 20 mwaka huu akiwa Usa River alsikika akisema: "Lowassa hana umuhimu wowote” kwenye kampeni hizo.

Kiongozi huyo alikuwa akichangia mjadala usio rasmi uliokuwa ukiwahusisha makada kadhaa wakongwe wa CCM, walipokuwa wakisubiri kuanza kwa msafara wa kwenda kwenye moja ya mikutano ya kampeni.

Monday 19 March 2012

DK. HARRISON MWAKYEMBE ARIPOTI OFISINI NA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO

Nauibu Waziri wa Ujenzi Dr Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ofisini kwake kuhusiana na maendeleo ya Afya yake nakusema kwamba yeye sasa yuko fiti kiafya, na ameripoti ofisini rasmi leo hii alipoulizwa maswali kutoka kwa waandishi wa habari akasema mambo yote anaichia serikali kupitia tume maalumu iliyoundwa kufutilia suala la ugonjwa wake

Sunday 18 March 2012

MWENYEKITI WA CCM KATA YA MBUGUNI AHAMIA CHADEMA

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa CCM wa Serikali ya Kitongoji cha Madukani, eneo la Msitu wa Mbogo, Kata ya Mbuguni,Godzed Minja, juzi amerudisha kadi ya CCM na kujiunga na CHADEMA, wakati makada wa chama hicho wakimnadi Mgombea wao Nassari wilayani humo.

Akizungumza mara baada ya kujiunga na CHADEMA, Mwenyekiti huyo Minja, alisema kuwa amefanya uamuzi huo kutokana na kuona CCM haina sera zaidi ya kusambaza matusi na kashfa badala ya kujibu hoja za msingi.

“Mimi naahidi nitakuwa mwana Chadema safi na mwaminifu na sitarudi nyuma katika mapambano haya, CCM imepoteza mwelekeo,’’ alisema Minja.

Alisema kuwa atatumia muda wake mwingi kuhakikisha CCM katika Kata ya Mbuguni inapotea kabisa kwa sababu hawana sera za kuwaeleza wananchi juu ya ugumu wa maisha waliyosababisha na kuchangia viongozi wa chama hicho kupata wakati mgumu kwa Wananchi.

Naye Mchungaji Israel Natse, akizungumza wakati akimnadi Mgombea wao, Nassari alisema kuwa eneo la Msitu wa Mbogo, Kata ya Mbuguni CCM imekwisha kwa sababu wanachama wengi wamehama chama hicho na kujiungana Chadema, kutokana na sera zao za matusi mbele ya watoto wadogo.

Alisema kuwa wanachama zaidi ya 300 wanasubiri Katibu wa chama hicho Taifa Dk. Slaa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, ili wakabidhi kadi hizo na kukabidhiwa kadi za Chadema mbele yao.

PIA Chadema yataka mdahalo huko Arumeru
Katika hatua nyingine Chadema, kimeomba kufanyika mdahalo wa wagombea wote wa ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ili kutoa fursa kubwa kwa wapigakura wa jimbo hilo na Watanzania kwa ujumla, kuwafahamu.

Meneja Mwenza wa kampeni wa Chadema, Vincent Nyerere, alitoa ombi hilo jana katika mikutano ya kampeni ya chama hicho, katika Kijiji cha Kikatiti na Maleu, wakati mgombea ubunge wa chama hicho, Nassari akiomba kura.

Nyerere ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, alisema uchaguzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki unasura ya kitaifa, hivyo ni busara kutoa fursa kwa Watanzania wengi kuwajua wagombea, sera zao na nini wamejipanga kuwafanyia wakazi wa jimbo hilo.

“Sisi Chadema tunataka wagombea wengine wakubali hasa CCM ambao wamekuwa wakikacha midahalo ili tutowe fursa kwa Watanzania kuwajua wagombea wao kwani kipindi cha kampeni ni kifupi sana, hivyo hakitowi nafasi wagombea kujulikana,”alisema Nyerere.

Awali Nassari aliwataka wakazi wa jimbo hilo kubadilisha siku ya kimataifa ya wajinga ambayo huadhimishwa Aprili mosi kila mwaka kuwa siku ya werevu kwa kuchagua kupinga maisha magumu, kupinga vitu kupanda bei na kupinga Meru kukosa ardhi na maji.

Nassari alisema, kumchagua yeye ni kuondoa shida na mateso yao yanayowakabili kutokana na serikali ya CCM kushindwa kutatua shida zao kwa miaka 50 sasa.

Mgombea huyo, aliendelea kusisitiza kuwa kati yawagombea wote, yeye ndiye anaishi Arumeru na ni mpiga kura wa jimbo hilo, hivyo anajua matatizo ya wakazi wa jimbo hilo.

“Mimi mimezaliwa Meru,nimesoma Meru,naishi Meru na ninafanya kazi Meru hivyo najua matatizo yenu na namna ya kuyatatua”alisema Nassari.

CHADEMA NA RADA UCHAGUZI MDOGO ARUMERU

Katika mikutano yao juzi na jana, Chadema kwa upande wake walitaka kukamatwa kisha kufikishwa mahakamani, wahusika wote wa ufisadi wa rada.

Meneja mwenza wa Kampeni za chama hicho jimboni Arumeru Mashariki, Vincent Nyerere, akizungumzia kurejeshwa kwa fedha za rada, alisema hoja sio kufurahia bali ni kuwafikisha mahakamani wote waliohusika na kununua rada kwa ulaghai, hivyo kujipatia mabilioni ya fedha.

“Hoja hapa sio kurejesha chenji eti zinunuwe madawati na vitabu, hoja ni hatua gani wanachukuliwa waliohusika na kununua rada ili kujipatia fedha ambazo zilisababisha watoto wao kusoma nje na watoto wa masikini kufa kwa kukosa madawa hospitali na kukaa chini?,”Alihoji Nyerere ambaye ni Mbunge wa Musoma Mjini.

Alisema ikiwa Serikali haitawakamata watuhumiwa wa ufisadi huo, basi wafungwa wote waliotiwa hatiana kwa makosa madogo madogo kama kuiba kuku, waachiwe.

Mbunge huyo pia alimgeukia Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa kwa kusema kwamba kiongozi huyo hana mamlaka ya kumzuia kumzungumzia baba yake,Hayati Julius Nyerere jukwaani kwani yeye si mwanafamilia bali ni msajili wa vyama.

Akizungumza katika mikutano iliyofanyika katika vijiji cha Ngarenanyuki na Msitu wa Tembo, Nyerere alisema Tendwa kama anataka awe mwanafamilia wa Nyerere kwa kuomba, afanye hivyo.

“Tendwa ni Msajili wa Vyama vya Siasa sio msajili wa koo, kama kazi ya siasa imemshinda basi awe msajili wa koo,”alisema Nyerere.

Mbunge huyo alisema alilazimika kutoa kauli nzito dhidi ya Mkapa baada ya kutoa taarifa ya uongo kuwa hamtambui kama mwanaukoo wa Nyerere.

Akizungumzia hoja ya Tendwa kuwa wakati wa kifo cha Mwalimu, yeye (Vincent) alikuwa mtoto, alimtaka Tendwa afanye uchunguzi na kuuliza wengine kwani yeye hakuwa mtoto wakati wa kifo cha Mwalimu na kwamba alikuwa na ufahamu wa kila kilichotokea wakati huo.

Ahadi za wagombea
Wakati viongozi wa Chadema na CCM wakiendelea kupimana ubavu majukwaani, wagombea wao Nassari na Sioi, sawia wameendelea kutoa ahadi za kutatua kero za wakazi wa Arumeru Mashariki ambao kilio chao kikubwa ni uhaba wa ardhi na maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na umwagiliaji mashamba.

Nassari katika ahadi zake juzi na jana alisema ikiwa atachaguliwa kuwa mbuge, atapeleka hoja binafsi bungeni kudai ardhi ya Meru ambayo kwa sehemu kubwa ipo mikononi mwa walowezi wachache.

Alisema zaidi ya ekari 13,000 zinamilikiwa na watu wachache ambao wameanzisha mashamba ya maua na kujenga viwanja vya gofu na farasi, huku wakizuia maji kufika katika makazi ya watu na badala yake maji hayo, kutumika kumwagilia uwanja na kuogeshea farasi.

“Leo hii kuna mashamba ya maua hapa, licha ya kukopeshwa na Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) Sh50 bilioni kwa udhamini wa Serikali, wameshindwa kulipa mishahara mizuri, badala yake wanawalipa ninyi kati ya Sh53,000 na 60,000 wakati pia afya zenu zinadhurika,”alisema Nassari.

Alisema pia atahakikisha anarejesha soko la Mbuguni, kutatua tatizo la maji na afya na pia kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali zao.

Kwa upande wake Sioi aliahidi kutekeleza ahadi zote zilizoachwa na mbunge aliyetangulia, ambaye ni baba yake mzazi, Marehemu Jeremiah Sumari.

Alisema atajikita kutatua tatizo la uhaba wa ajira kwa vijana ndani ya jimbo hilo kwa kushirikiana na Serikali bega kwa bega ikiwa ni pamoja na kuzindua vituo vya ujasiriamali kwa vijana ili waweze kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa serikalini.

“Nichagueni ili niweze kukamilisha ahadi zote zilizotolewa na mbunge aliyetangulia, nitajikita kutatua tatizo la ajira kwa vijana kwa kushirikiana na Serikali bega kwa bega,” alisema Sumari.

WASSIRA AMVAA DR WILBROD SLAA

Dk Slaa anatua Arumeru kipindi ambacho anasubiriwa kujibu tuhuma zilizotolewa na Wassira ambaye pia ni mlezi wa CCM mkoa wa Arusha.

Wassira katika mikutano mbalimbali ya kumnadi Sioi juzi na jana, alidai kwamba Dk Slaa anawajibika kuwajibu Watanzania sababu za kufukuzwa kwake ukasisi ndani ya Kanisa Katoliki, kabla ya kuingia kwenye siasa.

Wassira alisema Dk Slaa ambaye amekuwa msitari wa mbele kukemea ufisadi nchini, si mkweli kwani alifukuzwa baada ya kutafuna fedha za ujio wa Papa John Paul – II aliyezuru Tanzania mwaka 1990, wakati huo Slaa akiwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

“Huyu Dk Slaa alitafuna fedha za ujio wa Papa miaka ya nyuma na ndio chanzo cha kufukuzwa upadri,tena haya hata nyie mlichanga hizo fedha kwenye vigango vya parokia si mnakumbuka,”alisema Wassira.

Wassira aliendelea kumtuhumu Dk Slaa kwamba anaendeleza ufisadi ndani ya Chadema kwa kile alichodai kwamba alimfukuza kazi mhasibu wa chama hicho, kwa kosa la kushindwa kumlipa mchumba wa Dk Slaa, Josephine Mushumbusi kiasi cha Sh10 milioni.

Wakati huo huo,Wassira ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, alisema kwamba mgombea ubunge wa Chadema,Joshua Nassari hafai kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kuwa ni kijana mkorofi na mara kwa mara, baba yake mzazi amekuwa akimsihi kuachana na ukorofi tangu wakati akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Alisema kwamba baba wa mgombea huyo ambaye ni kiongozi wa dini, amekuwa akimsihi kuachana na ukorofi ikiwa ni pamoja na kuoa ili aweze kutulia lakini cha ajabu, Nassari amekuwa akionekana na bibi wa kizungu mwenye umri wa zaidi ya miaka 60 akizunguka naye mitaani jijini Arusha.

Wakati Wassira akitoa kauli hiyo, baba yake Nassari, Mchungaji Samuel Nassari na mkewe walihudhuria uzinduzi wa kampeni za mtoto wao zilizofanyika Jumamosi ya wiki jana kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Leganga, Usa River.

Lowassa,Mbowe vitani Arumeru

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema), Freeman Mbowe amesema chama chake kinamgonja kwa hamu Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa katika kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha.Kauli ya Mbowe inatokana na habari zilizoenea Arumeru ambazo pia zimethibitishwa na watu walio karibu na Lowassa, zikisema Mbunge huyo wa Monduli (CCM) wakati wowote atatua Arumeru Mashariki kumpigia kampeni mgombea wa chama chake, Sioi Sumari.

“Mzee (Lowassa) ni kweli kwamba ana mpango wa kuja hapa kumpigia kampeni mgombea wetu wa CCM, inaweza kuwa ni wiki ijayo au wiki ile nyingine, nadhani bado anajipanga. Ila taarifa za uhakika ni kwamba atakuja,”alisema mmoja wa makada wa CCM jana asubuhi.

Taarifa za kwamba Lowassa atashiriki kwenye kampeni hizo zilianza katikati ya wiki hii siku chache kabla ya kurejea kutoka Ujerumani.

Kwa upande wake, Lowassa akizungumza na Mwananchi kwa simu jana, hakuthibitisha wala kukanusha taarifa hizo, zaidi ya kusema kwamba hivi sasa anapumzika baada ya kurejea kutoka nchini Ujerumani alikokwenda kwa ajili ya matibabu ya macho.

“Kwani vipi……kwa kweli kwa sasa siwezi kusema lolote kuhusu hilo, ndiyo kwanza ninapumzika kama unavyojua nimetoka safari, katika hilo tusubiri kwanza,” alisema mbunge huyo ambaye anatajwa kwamba alikuwa akimuuga mkono Sioi kuanzia kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM.

Kwa upande wake Mbowe akizungumzia taarifa za ujio wa Lowassa alisema: “Tunamsubiri sana kwa hamu, kwani yeye ni nani? Lowassa ni kama mtu mwingine yoyote ndani ya CCM, hivyo yoyote atakayeletwa na CCM wala hatumwogopi, tuko tayari kukabiliana naye.”

Aliongeza: “Kwani Mkapa (Benjamin) si alikuja hapa….akamuulize baada ya kuzindua kampeni za chama chake na kusema maneno yake kilichomtokea ni nini? Kwa hiyo bwana na yeye (Lowassa) ni walewale maana hana tofauti na Mkapa maana wote wanatoka CCM, sisi Chadema hatutishiki hata kidogo.”

Lowassa ni miongoni mwa wazaliwa wa mkoani Arusha wanaotajwa kwamba wanakubalika katika siasa za Arumeru, hivyo ujio wake unaweza kuwa chachu kubwa katika kampeni za CCM kinachopigania kuendelea kushika nafasi ya uwakilishi wa jimbo hilo.

Wakati hayo yakiendelea, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa anatarajiwa kutua Arumeru leo kuongeza nguvu katika kampeni za Chadema ambacho kinawania kujenga heshima kwa mgombea wake, Joshua Nassari kutwaa jimbo hilo.

Tayari CCM wameongeza nguvu za kampeni zake kwa kuwaogeza makada kadhaa, wengi wakiwa ni wabunge wa majimbo mbalimbali wanaoongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira, hivyo kuongeza chachu ya kampeni hizo.

Thursday 15 March 2012

TEPE ZA HIV NCHINI TANZANIA ZA KELA

Wanaharakati nchini Tanzania wameelezea kughadhabishwa na hatua ya baadhi ya shule nchini humo kuwataka wanafunzi wanoishi na virusi vya HIV kuvaa riboni nyekundu kwenye sare zao za shule wakiwa shuleni.Mwalimu mkuu wa shule moja ameambia BBC kuwa kitendo hicho kilifanyika kufuatia ombi la wazazi kuhakikisha kuwa wanafunzi wagonjwa hawapewi majukumu ambayo huenda yakaathiri afya yao.
Lakini ubaguzi kama huu unakiuka sheria ambao adhabu yake ni kifungo cha miaka mitatu gerezani kulingana na shirika moja la kutetea haki za waathirika wa HIV.Waziri wa afya amesema hawezi kutoa tamko lolote kuhusu madai hayo hadi uchunguzi utakapofanywa.Kulingana na shirika la UNAids, takriban asilimia tano ya watu milioni 1.4 nchini Tanzania, wanaishi na virusi vya HIV.

BREAKING NEWS.....VINEGA KORTINI

.Kundi la ANTI-VIRUS watamka wazi kuhusu kesi AMBAPO KUSAGA ANAWASHITAKI MAPACHA KWENYE KESI YA MADAI AMBAYO KILA MMOJA WETU ANASHANGAA KWANI WAO NDIO WAKUSHTAKIWA.  tarehe 21 mwezi 3 mwaka 2012,,saa 7 mchana pale mahakama ya hakimu mkazi kisutu,juu ya baadhi ya vinega YAANI MAPACHA!AMBAO WAMESHTAKIWA NA MMILIKI WA KITUO HICHO CHA CLOUS FM,ambapo vinega wa ANT-VIRUS walikumbushana kukutana "vinega wote mnaombwa kwenda kushuhudia na kusikiliza madai ya WAFU FM!SO ukiwa kama unapenda kusikiliza jinsi vinega wanavyotuhumiwa" hiyo ni kauli yao kwa pamoja.pia wameongeza ya kwamba kwenda kuisikiliza kesi yao ni bure "ni bure usisite na ni haki yako pia kusikiliza kinachoendelea".pia wao wanadai washangaa suala Kusaga kuwashitaki Mapacha mmoja wao ameandika ya kwamba wanauzunika "ambapo

Tuesday 13 March 2012

BROKEN HEART DANCE by SOLO THANG ft NIAMH CHAMBERS(OFFICIAL VIDEO)

After releasing "I AM TRAVELLAH vol 1" On Jan 2012, on ITUNES***,,SOLO THANG aka TRAVELLAH is NOW working on his New Project,Vol 2,,with this song BROKEN HEART

Friday 9 March 2012

STARTING SCHOLARSHIPS

Get Scholarship Updates
The Small List of Scholarships below change on a regular basis. To make it easier to find next time you may want to bookmark this page.
In order to receive information about new scholarships that become available throughout the year you should Register for a Free Account. It's Fast and Easy....or for a copy of our newsletter, click here for the Word Document.

Thursday 1 March 2012

MVUA YA UPEPO MKALI YANYESHA WILANI KYELA

Mvua iliyoambatana na kimbunga ilizonyesha jana ya tarehe 29 februari imesababisha maafa hapa wilayani, karibia nyumba nyingi zimeezuliwa mabati likiwemo kanisa kubwa la morovian lililopo kijiji cha Ibungu. Habari ikiripotiwa toka eneo lililopo kanisa hilo nami nikiwa shuhuda wa tukio hilo ni kwamba tatizo kubwa lililosababisha kanisa kuezuliwa ni kwasababu ya kutomaliziwa kwa  madirisha yake. Baada ya tukio hilo niliweza kukuta na Mchungaji Mzee Mwakyalo alisema yeye binafsi anasikitishwa sana na kuezuliwa kwa kanisa hila alisisitiza ya kwamba kila mtumishi wa kanisa hilo aweze kuvumilia hali iliyotokea kwani ni mipango ya mungu.
Mimi binafsi niliweza kusikitishwa na hali ya hewa iliyotokea siku ya jana, lakini ningelipenda kusisitiza hili la kuezuliwa kwa kanisa hili, tatizo sio tu la madirisha kutokamilika bali ni “ukwasi”. Kwani hili ndilo tatizo kubwa la makanisa yaliyopo vijijini kwani vijana na wazee ambao niwaumini wa makanisa hayo huwa wanajituma sana kufyatua tofali za kujengea makanisa hayo lakini mwisho makanisa mengi huanguka na kuwa magofu. Jambo la muhimu kwa makanisa haya ambayo yana maaskofu na viongozi mbalimbali wasiangaliwe huduma hii kwa undani bila kusahau vijijini na sikuangalia mijini tu ambako ndiko viongozi wetu wa dini wanakojenga makanisa huku wengi wakidai nikutokana naongezeko la watu na kuifanya huduma kumfikia kila mtu.
Wakati huohuo katika eneo la mikumi imeripotiwa kuvunjika tawi la mti na kuua ng’ombe mmoja, pia maeneo  mbalimbali kumetokea uharibifu mkubwa wa mazao kama migomba na mahindi kuanguka.

LATEST NEWS

Share

Widgets

Total Pageviews