Mvua iliyoambatana na kimbunga ilizonyesha
jana ya tarehe 29 februari imesababisha maafa hapa wilayani, karibia nyumba
nyingi zimeezuliwa mabati likiwemo kanisa kubwa la morovian lililopo kijiji cha
Ibungu. Habari ikiripotiwa toka eneo lililopo kanisa hilo nami nikiwa shuhuda
wa tukio hilo ni kwamba tatizo kubwa lililosababisha kanisa kuezuliwa ni
kwasababu ya kutomaliziwa kwa madirisha yake.
Baada ya tukio hilo niliweza kukuta na Mchungaji Mzee Mwakyalo alisema yeye
binafsi anasikitishwa sana na kuezuliwa kwa kanisa hila alisisitiza ya kwamba
kila mtumishi wa kanisa hilo aweze kuvumilia hali iliyotokea kwani ni mipango
ya mungu.
Mimi binafsi niliweza
kusikitishwa na hali ya hewa iliyotokea siku ya jana, lakini ningelipenda
kusisitiza hili la kuezuliwa kwa kanisa hili, tatizo sio tu la madirisha
kutokamilika bali ni “ukwasi”. Kwani hili ndilo tatizo kubwa la makanisa
yaliyopo vijijini kwani vijana na wazee ambao niwaumini wa makanisa hayo huwa
wanajituma sana kufyatua tofali za kujengea makanisa hayo lakini mwisho
makanisa mengi huanguka na kuwa magofu. Jambo la muhimu kwa makanisa haya
ambayo yana maaskofu na viongozi mbalimbali wasiangaliwe huduma hii kwa undani
bila kusahau vijijini na sikuangalia mijini tu ambako ndiko viongozi wetu wa
dini wanakojenga makanisa huku wengi wakidai nikutokana naongezeko la watu na
kuifanya huduma kumfikia kila mtu.
Wakati huohuo katika eneo la
mikumi imeripotiwa kuvunjika tawi la mti na kuua ng’ombe mmoja, pia maeneo mbalimbali kumetokea uharibifu mkubwa wa mazao
kama migomba na mahindi kuanguka.
No comments:
Post a Comment