Social Icons

Thursday 16 February 2012

WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) WAFANYA MITIHANI YAO YA MWISHO MWA SEMISTA GIZANI


LEO hii karibia asilimia kubwa ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Udom wafanya mitihani yao ya mwisho ya semista gizani, hii nikutokana na kukatika kwa umeme, ili limewatokea wanafunzi wale ambao walikuwa na mitihani jioni ya usiku huu wa tarehe 17 februari na wengi wao walikuwa ni wale wa mwaka wa tatu.
Wakati hili likitokea utawala wa chuo waliamua kutoa taarifa TANESCO , ambao walihaidi kurudi kwa umeme baada ya dakika chache, walimu wa kozi husika walitoa angalizo kwa wanafunzi
kwamba wasubiri umeme utarudi lakini haikuwa hivyo walivyotarajia kwani umeme haukurudi kwa wakati. Ndipo ulichukuliwa uhamuzi wa walimu kwamba wanafunzi ambao hawakumaliza mitihani waweze kukusanya mitihani na vijitabu vya kujibi mitihani ili kurinda hadhi ya mitihani na kuepuka uhalisia wa mitihani hiyo(validity and reliability of exams) kwa kweli huo ndio ukweli halisi maana giza lilianza kuwa kubwa kwenye vyumba vyote vya mitihani. Ndipo wanafunzi walipoweza kukusanya mitihani na vijitabu vya kujibia mitihani.
Baada ya muda mchache umeme ukarudi na ni baada ya wanafunzi kutoka, wakati huo huo chuo cha elimu tatizo lilikuwa hilo hilo, ampapo inaripotiwa ya kwamba umeme ulipo rudi kama nusu saa hivi Tangazo lilitolewa ya kwamba kwa wale wanafunzi walioweza kufanya mtihani wa “utafiti katika elimu” ya kwamba wasiondoke na kwenda makwao hadi uamuzi utakapo chukuliwa wa nini kifanyike. Lakini hadi sasa wanafunzi wengi wameweza kuondoka chuoni hapo na hiyo ni baada ya kutoka kwenye mtihani na pia na wengine wanategemea kuondoka hasubuhi kwani wengi wao waliweza kukata tiketi mapema kwenda makwao, hadi dakika ya mwisho chanzo cha habari hizi kinasema wanafunzi wengi hawakubaliani na tangazo hilo maana wengi wao tayari wameshaondoka na hawapo tena chuoni na wengine wameishakata tiketi tayari kwa safari.
Lakini penye jambo pia kuna ukinzani wengine walitoa mapendekezo ya kwamba mitihani yote iliyofanyika muda huo iweze kurudiwa wamependekeza hivyo.wamesema haina budi kufanya hivyo pamoja na kwamba ni gharama kubwa kurudia na kukidhi gharama za mitihani hiyo.
Hadi tunafikia tamati, jibu la nini kifanyike halijulikani hadi uamuzi kamili utakapo tolewa kesho na wakuu wa idara husika.

No comments:

LATEST NEWS

Share

Widgets

 

Total Pageviews