Social Icons

Saturday 25 February 2012

TAMKO LA VINEGA JUU YA MAKUBALIANO YA SUGU NA RUGE


Juzi ya tarehe 23 ya mwezi February, 2012 mida ya saa 1 usiku mpaka saa 5 na nusu usiku katika eneo la Mwenge Vinega wa anti virus tulikutana katika kufanya tathmini na kujadli maridhiano ya kumaliza ugomvi wa kimaslahi kati ya Kundi la Vinega na Redio Clouds pamoja na Bwana Rugemalila Mutahaba,katika kikao hicho tuliridhiana kutoa tamko hili kwa umma wote wa watanzania na wapenda maendeleo wote wa sanaa yetu.
"Ni kweli hakunaga Vita isiyo na mwisho lakini pia katika kila vita malengo ya msingi yanapaswa kuwa mbele na daima mbele...Harakati hizi za Anti virus zilipoanza wengi tulionekana kama wasaliti na wapuuzi,wahuni na kuonekana kama tuna wivu tu na mafanikio ya baadhi wa wadau ila daima tulisimama katika kweli na hatimae Umma/jamii ya watanzania ukasikia sauti na hoja zetu na kuona kweli tuna mambo ya msingi,Hoja zetu mbele ya umma ndio ilikuwa silaha ya vita hii ya Anti virus na wala si nguvu ya Propaganda na uzushi...Tumepiga makelele na hatimaeTaifa zima wakaona kweli hapa kuna hoja na zinapaswa kuzingatiwa na wala si ugomvi wa mtu mmoja bali ni harakati za kweli za kukomboa sanaa yetu na kuvunja ile mifumo ambayo siyo sahihi inayoendelea kunyonya jasho la wasanii wa Tanzania na kuwafanya kuwa mafukara na wasio na mategemeo na kupelekea kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya na hatimae kufanya mambo ya kihalifu.Sanaa hii kwa muda imekuwa ikihodhiwa na watu wachache na kujitajirisha na kuacha lundo la wasanii kuishi maisha mabovu.Dhamira yetu ni kumaliza kabisa mifumo hii mibovu ambayo tunaamini ikimalizwa msanii wa kitanzania ataweza kupata kipato na kujiajiri na kuendesha maisha yake sawasawa.

Friday 24 February 2012

Precision Air yabadili ratiba ya Afrika Kusini



SHIRIKA la Ndege la Precision Air, limetangaza kufanya  mabadiliko katika ratiba yake ya safari kwenda Johannesburg nchini Afrika Kusini, ambapo itaanza kuondoka saa 11 jioni badala ya saa mbili usiku ili kuwawezesha wasafiri wake kuwahi na kuwapatia urahisi wa kuunganisha safari kwenda kwingine.

Akizungumza katika makao makuu ya Precision Air, Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Patrick Ndekana alisema uamuzi huo umekuja baada ya utafiti uliofanywa na shirika hilo, uliopendekeza watumiaji wa huduma hiyo wanapendelea kusafiri mapema ili kupata urahisi wa kuunganisha safari kwenda kwingine pamoja na kujihakikishia usalama kwa wanaoishia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Oliver Tambo.

Haji Salum ‘Mboto’: Mr Bean wa Bongo mwenye ndoto ya kung’aa kimataifa


 KATIKA fani ya uigizaji, mbali na kipaji lakini pia namna msanii anavyobeba uhusika wa nafasi anayoigiza huwa ni mambo yanayomvutia mtazamaji.

Uwezo wa msanii utapimwa kutokana namna alivyoweza kuuvaa uhusika mfano anapotakiwa kuigiza kama ana huzuni lazima aoneshe hali ya huzuni, kama anaigiza tajiri aonekane kweli tajiri, kichaa kweli aonekane mgonjwa wa akili na kama anapaswa kuwa mchekeshaji basi awe mchekeshaji kweli. 
Uwezo wa kubeba uhusika vizuri ndio huko kunakomfanya msanii wa vichekesho Haji Salum maarufu kwa jina la Mboto kuweza kung’ara katika fani ya filamu za vichekesho. Anasema, “Ninakuwa na wakati mgumu sana wakati wa kuandaa kazi, tunalazimika kurudia mara kwa mara.

Tuesday 21 February 2012

What Is Extreme Poverty Like?

EXTREME poverty is life threatening. It means not having enough food, water, and fuel as well as lacking adequate shelter, health care, and education. It affects one billion people, roughly the equivalent of the entire population of the Americas. Yet, most people in places like Western Europe and North America have never known a person in extreme poverty. So let us meet some now.

Mbarushimana lives in Rwanda, Africa, with his wife and five children. A sixth child died of malaria. He says: “My father had to divide his land among six of us. My share was so small that I had to move my family to a town. My wife and I work at carrying sacks of stones and sand. Our home has no windows. We get water from a well at the police station. We usually have one meal a day, but when there is no work, we have no food all day. I go out when that happens—I can’t bear listening to the children when they cry for food.”
A poor family in Bolivia getting water from a river Read More

Thursday 16 February 2012

WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) WAFANYA MITIHANI YAO YA MWISHO MWA SEMISTA GIZANI


LEO hii karibia asilimia kubwa ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Udom wafanya mitihani yao ya mwisho ya semista gizani, hii nikutokana na kukatika kwa umeme, ili limewatokea wanafunzi wale ambao walikuwa na mitihani jioni ya usiku huu wa tarehe 17 februari na wengi wao walikuwa ni wale wa mwaka wa tatu.
Wakati hili likitokea utawala wa chuo waliamua kutoa taarifa TANESCO , ambao walihaidi kurudi kwa umeme baada ya dakika chache, walimu wa kozi husika walitoa angalizo kwa wanafunzi

Thursday 9 February 2012

MATOKEO KIDATO CHA NNE YAVUNJA MOYO KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU !

Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Joyce Ndalichako, Baraza limefuta matokeo ya watahiniwa hao, ambao kati yao, 3,301 ni wa Mtihani wa Kidato cha Nne na wawili ni wa Maarifa (QT). Mwaka juzi, wanafunzi 303 walibainika kufanya udanganyifu huo. Aidha, watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 wamefaulu mtihani wa huo, wakiwamo wasichana 90,885 sawa na asilimia 48.25 ya wasichana waliofanya mtihani na wavulana ni 134,241 sawa na asilimia 57.51 ya wavulana waliofanya mtihani huo.

Mwaka juzi, watahiniwa waliofaulu walikuwa 177,021 sawa na asilimia 50.40 ya watahiniwa waliofanya mtihani huo, hivyo kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 2.63. Dk. Ndalichako alifafanua aina ya udanganyifu wa watahiniwa hao na kusema zaidi ni 2,896 wamefutiwa matokeo kwa sababu ya kuwa na mfanano wa majibu usio wa kawaida. Alisema wadanganyifu wengi wanatoka Mwanza na Arusha.

Alizitaja aina nyingine za udanganyifu na idadi ya watahiniwa waliohusika kwenye mabano, kuwa ni waliokamatwa na wasimamizi ndani ya chumba cha mitihani wakiwa na ‘notes’ (182); waliofanyiwa mitihani na watu wengine (3); waliosajiliwa kufanya mitihani kwa kutumia majina ya wengine wakati walishafanya mtihani (4) na waliokuwa na karatasi za majibu zenye miandiko tofauti au kuwa na miandiko tofauti katika karatasi ya somo moja (155).

Mgomo wa madaktari, Suluhu yapatikana baada ya mazungumzo.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewasimamisha kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali Dokta Deo Mtasiwa ili kupisha uchunguzi kuhusu chanzo cha mgomo wa Madaktari unaoendelea.
Hata hivyo Waziri Mkuu Pinda amemwachia Rais Jakaya Kikwete uamuzi wa mwisho kuhusu hatma ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dokta Haji Mponda na Naibu wake Dokta Lucy Nkya ambao pia wanalalamikiwa na Madaktari kwa madai ya kupuuza malalamikoyao.
Mapambazuko ya asubuhi ya Alhamisi yanamkuta Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili lengo kuu likiwa ni kutatua mgogoro baina ya serikali na madaktari.
Ni siku ya 17 tangu mgogoro huo uanze na mashinikizo yamekuwa yakiongezeka kila kona huku kukiwa na tetesi kuwa baadhi ya Mawaziri walimtaka mwenzao Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dokta Haji Mponda kujiuzulu kutokana na sakatahilo.
Waziri Mkuu amefika katika hospitali hiyo majira ya saa 3 asubuhi huku mamia ya madaktari wakimsubiri kwa hamu kujibu madai waliyomuwasilishia mezani likiwemo lile la kuwawajibisha viongozi wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa madai ya kutowasikiliza na kuwapuuza pindi wanapowasilisha madaiyao.
Miongoni mwa madai ya madaktari hao ni kupewa kipaumbele kwa madaktari walio kwenye mafunzo kwa vitendo, kuongezewa posho za muito wa ziada yaani (on call allowance), Posho za nyumba au kupewa nyumba, posho za mazingira hatarishi, usafiri na kuongezewa mshahara.
Pamoja na yote aliyowaahidi Waziri Mkuu ametoa mwito kwa madaktari hao kurejea kazini ili kuwasaidia wagonjwa wanaoteseka kwa kukosa hudumayao.
Mbali na masuala ya mishahara Waziri Mkuu pia ameahidi kuboresha mazingira ya kazi, mazingira ya afya mahospitalini, kuongeza vitendea kazi na kuwaongezea posho za mwito wa dharura yaani (on call allowance) kutoka shilingi 10,000/- mpaka shilingi 25,000/-.
Masuala mengine yasiyotatulika kwa haraka, Waziri Mkuu ameyaundia tume ya watu 9 itakayofuatilia na kumpelekea ripoti, tume hiyo imeshirikisha wawakilishi kutoka Chama cha Madaktari MAT, Chama cha wafanyakazi wa serikali kuu na afya TUGHE, mwakilishi kutoka Hazina, Wizara ya Afya na idara zingine kutoka serikalini na vyama vya wafanyakazi.
Kwa upande wao madaktari wameomba wapewe muda mzuri zaidi kwa ajili ya kuendelea kujadili masuala mbalimbali yanayowakabili.
Hata hivyo mpaka kikao kinamalizika madaktari hao wamekubaliana kusitisha mgomo na kurejea kazini kwa ajili ya kuendelea na kazi huku wakitarajia kukutana tena Mwezi ujao tarehe 3 mwaka huu kuangalia masualayaoya kikazi.
Mgogoro huo uliochukua takriban wiki tatu mfululizo umeanza baada ya Wizara ya afya kuchelewesha posho za Madaktari Wanafunzi hatua iliyowafanya wasitishe huduma katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuanza kuitisha vikao kupitia kwa Chama cha Madaktari Tanzania MAT ambavyo viliibua madai mengine ya nyuma.

Tuesday 7 February 2012

NALO HILI MUHIMU, KUUTAZAMA ULIMWENGU !


  •    BARACK OBAMA, RAIS WA MAREKANI
“Kuwa Rais kunamsukuma aone uhitaji wa kusali”- Katika hili tunamhitaji kiongozi mwenye misingi ya dini na mwenye kuamini.

  • ·        LA NACION, ARGENTINA
“Walipoulizwa wachague njia ya kuonyesha uzalendo wao, asilimia 56 ya waargentina wenye umri wa kati ya miaka 10 na 24 walisema kwamba wangependa kuvalia jezi ya timu ya kandanda ya Taifa”.-. Hapa kuna jambo la msingi tunaweza kujifunza watanzania. Je sisi kama wazalendo watimu yetu ya Taifa, hili kwetu tumekuwa waraibu tuko tayari kuvaa jezi ya Brazil nakuacha jezi zetu.

  • ·        SHIRIKA LA CHAKULA NA KILIMO LA UMOJA WA MATAIFA, ITALIA.
Matokeo ya utafiti Fulani yalidokeza kwamba “inakadiriwa kwamba asilimia 33 ya chakula kinachozalishwa ulimwenguni pote kwa ajili ya wanadamu hupotea au kutupwa, na hiyo ni kama jumla ya tani bilioni 1.3 kwa mwaka”

  • ·        PATRIARRCH KRILL, MKUU WA KANISA LA OTHODOKSI LA URUSI.
Siku hizi, vita na ripoti za vita zimeenea ulimwenguni pote kwa mfano Misri, Libya Somalia n.k, kwa hiyo jeshi la nchi yetu lazima liwe tayari siku zote kuwalinda watu wake na kila kitu ambacho tunaona kuwa ni kitakatifu kutokana na maadui wanaotoka nchi nyingine.

  • ·        PRESSEPORTAL, UJERUMANI.
Kiwango cha juu cha kabisa aksidenti za magari kilichoripotiwa kwa kampuni moja ya bima nchini ujerumani katika mwaka wa 2010, kilionesha kwamba aksidenti hizo zilitokea kati ya saa mbili asubuhi. “Mojawapo ya njia muhimu zaidi ya kuzuuia aksidenti ni kuwa na wakati wa kutosha wa kusafiri unapoelekea kazini asubuhi,” anasema afisa wa kampuni hiyo.

Saturday 4 February 2012

Wabunge wazuiwa kujadili mgomo wa madaktari

WABUNGE leo wamezuiwa kujadili kauli ya Serikali kuhusu namna ilivyoshughulikia mgomo wa madaktari.

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, amewaeleza wabunge kuwa, si busara kuijadili kauli hiyo kwa kuwa wamesikia upande mmoja tu wa Serikali, hawajasikia upande wa madaktari wanasema nini.

Ndugia amekiri kwamba suala ni nyeti kwa kuwa linahusu maisha na uhai wa wananchi wanaohitaji tiba lakini taratibu za uendeshaji wa mabunge ya Jumuiya ya Madola haziruhusu kujadili kauli za mawaziri mara tu baada ya kuwasilishwa.

Amesema kutojadili kauli hizo moja kwa moja kunaepusha kauli tofauti tofauti.

Kwa mujibu wa Ndugai, si busara kwa wabunge kuijadili kauli ya Serikali iliyowasilishwa leo bungeni na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda.

Ndugai amesema , madaktari hawajasikilizwa na hawawezi kwenda bungeni kutoa kauli yao lakini licha ya madai mengine, wanawatuhumu watendaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii hawawajibiki na wanatoa kauli za kashfa hivyo si busara kwa wabunge kulijadili suala hilo.

“Sijui kama tutakuwa tunajitendea haki hata sisi wenyewe unless ( isipokuwa) kama tupo informed (kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu jambo fulani” amesema Ndugai.

Ametoa msimamo huo wakati anatoa mwongozo wake kuhusu hoja ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) ya kuomba Bunge lijadili kauli ya Serikali kuhusu namna ilivyoshughulikia mgomo wa madaktari.
Mnyika amesema, ni busara kwa wabunge kuijadili kauli hiyo kwa kuwa, Serikali ni moja ya pande zinazohusika kwenye mgororo huo,hivyo ni busara kauli iliyotoa ijadiliwe na wahusika wawajibishwe.
Mbunge huyo aliomba mwongozo huo kabla Waziri Mponda hajawasilisha kauli hiyo, na baada ya kuwasilishwa, Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR- Mageuzi), na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema) nao waliomba kauli ya Serikali ijadiliwe. Baada ya Ndugai kutoa mwongozo huo aliiagiza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii izungumze na Serikali na madaktari ili kumaliza mgogoro huo.

Ameitaka kamati hiyo hiyo ifanye kazi hiyo haraka na itoe taarifa kuhusu yaliyojiri kwenye mazungumzo hayo na ushauri wa Bunge kwa pande husika.
Amesema, ushauri wa Bunge kwa pande hizo si lazima yawe maagizo, na kwamba, wabunge wanaruhusiwa kuhudhuria vikao vya kamati na pande husika, na kuchangia.

Friday 3 February 2012

CRDB yaipa Minaki milioni 5/-.

 BENKI ya CRDB imekabidhi sh milioni 5, kwa Shule ya Sekondari ya Minaki ili zitumike kwa ajili ya kuendeleza elimu shuleni hapo. Msaada huo ulitolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dorah Ngarija, wakati wa mahafali ya 52 ya shule hiyo, akisema kiasi hicho kimetolewa kwa lengo la kutatua baadhi ya kero zinazoikabili shule hiyo.

Alisema benki hiyo imekuwa ikitoa mchango mkubwa kwa sekta ya elimu, ikiwemo ya kutoa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ili kupata uzoefu wa kikazi.
Dorah alisema CRDB imefanikiwa kuwapelekea huduma za kibenki wanafunzi wa elimu ya juu ili waendelee kupata huduma za fedha wakiwa vyuoni.

Aliutaka uongozi wa shule hiyo kuendeleza historia iliyoachwa ya kuwa chanzo cha kutoa wanafunzi ambao baadaye watakuwa viongozi bora wa baadaye. Awali, mkuu wa shule hiyo, Arnold Chungu, alisema licha ya shule hiyo kuwa kongwe inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama uhaba wa vifaa, maji safi na salama ya kunywa.

Source: Tanzania Daima

Thursday 2 February 2012

Madini ya chuma yaleta maafa Nigeria

Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limesema kuwa shughuli ya uchimbaji dhahabu kaskazini mwa Nigeria imewasababishia maelfu ya watoto maradhi mabaya zaidi kutokana na uchafuzi wa madini ya chuma.

Human Rights Watch inasema kuwa uchafuzi huo ndio mbaya zaidi kuwahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni na watoto wengi katika eneo hilo wanahitaji msaada wa kimatibabu. Shirika hilo linasema tayari watoto mia nne wamekwishaaga dunia kutokana na mkasa huo. Baadhi ya watoto hao ambao wana umri wa miaka minane wanafanya kazi katika migodi ya dhahabu katika jimbo la Zamfara.

Viwango vya uchafuzi wa madini ya chuma ni vya juu zaidi katika baadhi ya vijiji na takriban asilimia arobaini ya watoto walioenekana kuwa na dalili ya kupata maradhi yanayotokana na uchafuzi huo wameaga dunia. Shirika la Human Rights Watch linasema kuwa uchimbaji wa madini unawaweka watoto hao katika hatari ya kuathirika na vumbi ya madini hayo ya chuma ambayo inachafua maji pamoja na chakula. Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa madini ya chuma husababisha matatizo ya kudumaa ubongo na umbo la watoto.Read More

Wednesday 1 February 2012

MWAKYEMBE:”NAMSHUKURU MUNGU KWA KUENDELEA KUNIPA NGUVU”

Kwa muda sasa,hali ya afya ya Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya,Dr.Harrison Mwakyembe, imekuwa ni gumzo lisiloisha.Yanasemwa mengi kuhusu ugonjwa unaomsumbua.Yeye mwenyewe hajaweka bayana juu ya ugonjwa wake.Serikali nayo,kwa kuzingatia taratibu za kitabibu,haiwezi kusema kitu.Bado anaugua.
Pamoja na kwamba bado anaugua,hali yake inaendelea vizuri.Mwishoni mwa wiki alithibitisha hilo pale alipoweza kuhudhuria ibada katika Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mch.Josephat Gwajima lililopo maeneo ya Kawe jijini Dar-es-salaam.

Anavyoonekana hivi sasa Dr.Harrison Mwakyembe



LATEST NEWS

Share

Widgets

 

Total Pageviews